Kuna mwenye uzoefu na matairi ya goodride?

Kuna mwenye uzoefu na matairi ya goodride?

kamanyora

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
209
Reaction score
133
Wakuu,naomba kuuliza kama kuna ambaye amewahi kutumia matairi ya goodride anielezee uimara wake,na je kwa masafa marefu kama kwenda musoma inaweza kupiga trip ngapi kwa private car,nilienda kununua matairi aina ya bridgestone nikakutana na haya matairi na nikaona bei yake iko chini ila mimi sijawahi kuyatumia,
 
Goodride kiukweli tairi ngumu kwa maana ya kutoboka ila kashata inapotea haraka sana..
Mi nlifunga mbele WESTLAKE nyuma GOODRIDE..GOODRIDE ilisha mapema ikawa kipara lakini pancha haipati traffik watakusumbua...
 
Asante mkuu kwa maoni hayo,unafikiri inaweza kuchukua miaka mitatu kabla traffic hawajaanza kusumbua?
 
Mkuu Mbona kuna mtu ananiambia anayatumia huu mwaka wa 3 toka aweke hazijamsumbua na anapiga nazo Safari sana!
Inawezekana maana zipo za aina nyingi,kuna zile za waya na za kawaida
 
Mkuu Mbona kuna mtu ananiambia anayatumia huu mwaka wa 3 toka aweke hazijamsumbua na anapiga nazo Safari sana!
Hazisumbui na ikiwa kipara haipati pancha mara kwa mara...Ila kashata zinaisha mapema...
 
Wasiwasi wangu ni kama hazijachakachuliwa. Ila niliwahi kutumia kwenye gari yangu kama miaka mitatu hivi. Hazikuwa zinavuma wala tatizo lolote la msingi. Ni tairi nzuri kwa maoni yangu.
 
Labda kama anafanya safari za kwenda vituo vya mafuta na kurudi nyumbani!

Mkuu amesafiri nazo mara 3 kwenda Musoma,Na mwingine nae Leo ambae namfahamu kabisa nimekuta kafunga nilivyomuuliza kasema amesafiri nazo mara nyingi sana Na huu Ni mwaka wa 4 hazimsumbui!
 
Wakuu,naomba kuuliza kama kuna ambaye amewahi kutumia matairi ya goodride anielezee uimara wake,na je kwa masafa marefu kama kwenda musoma inaweza kupiga trip ngapi kwa private car,nilienda kununua matairi aina ya bridgestone nikakutana na haya matairi na nikaona bei yake iko chini ila mimi sijawahi kuyatumia,
Habari ya mjini ni LingLong kaka. Weka mbali na watoto. Nimenunua nimeetembea nalo Km 7400 had I sasa ila dah zipo gado
 
Zinauzwaje kiongozi
120,000/= moja mkuu gerezani pale. Nipo mkoa kwasasa ila kuna fundi anajua vema tairi kuzichagua maana nyingine mbichi na pia anajua kuzifunga. If you want his contacts I can help

Note: Gari yangu ni Crown
 
Siyo mbaya mkuu nipe hiyo namba...
 
Mimi nilinunua 4 miezi mitatu iliyopita, tatu zimevimba pembeni, ila zinapiga mzigo na karibia kila wiki nina masafa ya dar moro kwenda na kurudi
 
Back
Top Bottom