The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Uwepo wa annunaks sio nadharia, rekebesha hapoUTANGULIZI:
Anunaki (ANUNNAKI) ni jina linalotokana na maandiko ya kale ya Sumeria, Akkadia, Ashuru na Babeli (eneo la Mesopotamia ya kale—leo ni Iraq).
Hawa Anunaki walikuwa miungu katika imani za watu wa maeneo hayo. Kuna maelezo mbalimbali kuhusu wao, lakini kwa ujumla, Anunaki walichukuliwa kama miungu wa Kale wa Mesopotamia waliohusishwa na maumbile, maadili, vita, na maamuzi ya binadamu.
Katika baadhi ya maandiko, Anunaki walionekana kama watoto wa mungu mkuu aitwaye Anu, ambaye alikuwa mungu wa mbinguni.
Walikuwa sehemu ya miungu ya juu waliokuwa wakiamua kuhusu maisha ya wanadamu na hatima ya dunia.
Katika karne ya 20 na 21, jina "Anunaki" lilianza kuhusishwa pia na nadharia za ajabu na zisizo na uthibitisho wa kisayansi, hasa kupitia kazi za watu kama Zecharia Sitchin, ambaye alidai kuwa Anunaki walikuwa viumbe wa kigeni (aliens) waliotoka sayari ya mbali aitwayo Nibiru.
Walikuja duniani maelfu ya miaka iliyopita na wakawa na mchango katika kuumba binadamu kwa kutumia uhandisi wa kijeni (genetic engineering).
Walidaiwa kuwafanya wanadamu kuwa wafanyakazi wao (slaves) wa kuchimba dhahabu na madini.
Nadharia hizi hazikubaliki kisayansi, lakini zimevutia watu wengi wanaopenda masuala ya siri, historia mbadala (alternative history), na nadharia za ajabu.
Anunaki ni sehemu ya historia ya kale ya mwanadamu kuhusu jinsi watu walivyoelewa ulimwengu. Wanaonyesha jinsi dini na hadithi zilivyotumika kueleza masuala ya asili, maisha, na kifo.
Leo hii, Anunaki wameingia pia katika filamu, vitabu, michezo, na mijadala ya mitandaoni kuhusu "viumbe wa kale wa anga".
Karibu sanaNipo kujifunza
Uko sahihiManeno ya tuliumbwa Kwa mfano wake kwenye vitabu vya dini yanatafakarisha sana hasa ukifanya comparison na hii stori pamoja na zile texts za miungu ya kihindi nk.
| ENEO | JINA LA MIUNGU & MAELEZO YAKE |
| Simeria | => ANUNNAKI * Miungu wa mbinguni na ardhini Misri Neteru Miungu kama Osiris, Ra, Isis |
| Misri, Neteru | => Osiris, Ra, Isis |
| Biblia | => Giants kama • Wana wa Mungu • Giants kama Goliath * (Genesis 6:1-4) Waliooa wanawake wa dunia, wakazaa majitu (Nephilim) |
| SOUTH AMERICA (Virococha) | => Quetzalcoatl * Miungu waliokuja na kuishi baharini au angani. • (kwa story ni kama NAMOR/AQUAMAN katika comics za Marvel/ DC. |
Kweli.
Kumbukumbu zilikuwepo. Wakoloni walizichukua zipo kwao katika majumba ya Musiums.Wenzetu waliweza kutunza kumbukumbu kupitia maandishi, na ndio maana hadi sasa tuna uwezo wa kujua historia zao.
Waafrika weusi tulichelewa sana!