Kuna nchi ukimpeleka mtoto kusoma chuo utajuta

Atokee mtu anipeleke nikasome USA
 
Kama mzazi unajiweza unapelekaje mtoto kusoma ASIA

ASIA yote inakimbilia Ulaya

Turudi kwenye mada

Nakubaliana na mtoa mada kwa sababu watoto wengi hawajalelewa katika mazingira ya kujitegemea
Ninamfahamu muhindi alimpeleka binti Malaysia, Baba akamchukulia apartment kakupa kila kitu, siku Ka 5 akakaa naye, akarudi Bongo.
Kutua airport, simu binti analia hatari, anaogopa hawezi! Baba akaingia gharama kumpeleka Kaka mtu, aende akakae wiki 2, azoee, Kaka alimiss chuo alikokuwa 2 weeks, ili amsaidie dada Ku settle!

Kweli hatulei watoto kujitegemea, wanakuwa tegemezi, kiasi wanaishia kuwa frustrated ulimbukeni wakipata Uhuru!
 
Watoto hawalelewi vizuri,wanafungiwa tu hata kujitegemea hawawezi,mtoto ukimuacha nyumbani peke yake mwezi mmoja tu anapigapiga simu na kuanza sijui kukimiss kuwa urudi nyumbani amechoka kuishi mwenyew,mzazi anamtafutia mtoto chuo nje akifikiri kuwa akiwa nje mtoto ataanza kujitegemea na kupata exposure fulani kumbe hamna msingi wwte wa maana aliomjengea mtoto kuhusu namna ya kuishi nje ya masomo...mtoto akiwa katika hali hiyo tu tayari mzazi ushapoteza,huko atakutana na watu kutoka mataifa mbalimbali ya watu wanaojielewa na waliokubuhu kupoteza wenzao huku wao baadaye wanakuwa safe,atakutana watu kutoka nchi kubwa wenye kariba ya majina kama Vladimir dobrovosky, Cheng Zhang, kina Khan Gandhi, Kina Pierre Olivier. Anakutana na Watoto wa dunia ya Kwanza wanaofahamu basics nyingi za maisha, watamfanyia mental manipulation hadi akirudi nyumbani mzazi utajiona mjinga sana...waandaeni watoto vizuri kabla kuwarusha abroad,mifano ipo mingi tu watu waliosoma nje na bado wako smart na wame add value kwenye maisha yao na ndugu zao kwa ujumla...
 
Nimetoka Kampala jumatano hapo,ulisemalo ni kweli,...Uganda sio nchi nzuri kwa watoto wa kike kusoma.
 
Mkuu nifanyie koneksheni ya kazi Basi inaonekana family yenu muko vizuri sana
 
Yan anatia huruma wazaz wake wamefariki wote yupo tu kwenye mjengo wao masaki hana hili wala lile na wenyewe wapo wawili mwenzake kabaki huko canada. Mwaka jana mama yao alikua kwenye life supporting machine yule wa canada akarudi amekaa wiki akawa anawaambia baba zake wakubwa mama atolewe machine ili afe ye arudi zake canada sasa sijui ni bahati nzuri au mbaya kabla kikao hakijakaa kama atolewe ile machine akafa jioni yake
 
Ivi unamfundishaje mutoto kujitegemea mkuu.? Yani mufano ni Kama kujipikia mwenyewe, au Nini ..na iyo inaanza akowa na umri gani mkuu
 
Aisee
 
Ivi unamfundishaje mutoto kujitegemea mkuu.? Yani mufano ni Kama kujipikia mwenyewe, au Nini ..na iyo inaanza akowa na umri gani mkuu
Vijijini wameimudu Sana hii. Tokea mtoto anavyokuwa akianza Tu kuelewa anatumwa islets chumvi, kaleta mwiko, taratibu akikua nenda mkachote maji, kaokoteni kuni, pikeni uji e.t.c

Mjini muache mtoto ataungua akipika,acha kukata nyanya utajikata, aacha kubeba ndoo utamwaga maji, Hamad kamaliza primary secondary kaenda boarding, akirudi dada mfulie mwanangu alikuwa shule, mpikie anapenda kuku, likizo imeisha alikuwa anaenda tuition Tu, anachojua ni kuoga. Chuo akajitegemee hawezi kukop!
 
Pamoja na ukweli kwamba si wote waendao huko wanakuwa chapombe lakini nadhani hiyo Vodka inapatikana kwa urahisi sana huko.
 
Aseeehhh!
 
Nadhani kutoka nje level ya masters si mbaya sana ,ila undergraduate Kuna shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…