Kuna nini nyuma ya ndoto hii? Naomba msaada

Kuna nini nyuma ya ndoto hii? Naomba msaada

Saoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2018
Posts
441
Reaction score
643
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Niende kwenye mada kuwa Leo nimeota tena kuwa nimegombana na mdogo wangu aliyenifata kufikia kiasi cha yeye kukimbia/kuhama kabisa nyumbani na kwenda kwa majirani kuomba msaada huku nikiwa sijui chanzo chake.

Wakati huohuo ninamuona bibi yangu mzaa baba huyu ni Marehemu lakini nashangaa yupo pale nyumbani na wala hanisemeshi chochote kuhusiana na ugomvi wa dogo langu ikumbukwe bibi huyu tayari nimarehemu(3yrs ago) kwakweli nimestuka mno na Home wazazi walikuwa wamesafiri tukabaki 3tu mimi, dogo na Bibi (ambaye tayari nimarehemu)

Wadau mwenye kujua tafsiri ya hii ndoto tafadhali pia ushauri nini nikifanye yasinitokee tena haya ndugu zangu?
 
Wewe kabila gani?maana ni kama asili yako inataka matambiko
 
wew ndio unanafas kubwa sana ya kuisaidia familia yenu na kuiondolea fedhea ya kuomba omba kwa watu ila kwakua hufanyi ivyo ndio mana weng wanaojua unauwezo wa kusaidia wamekaa kmya kukuangalia busara na uwezo wako utaishia wap kama leo wazaz wapo huna unachofanya wakiondoka itakuaje... kwa uwezo wangu nmeishia apo
 
Acha ujinga hizo ni ndoto tu.
Nakazia...

Kama ingekuwa ni hivyo kila siku watu wangekuwa hawafanyi kazi zingine kazi kufasiri ndoto tu... maana ndani ya sekunde moja mtu anaota ndoto ya masaa kadhaa (ndani ya sekunde unaota umekimbizwa na mende ukakimbia mpaka ukachoka ukatumbukia shimoni ukatoka kwa kuteleza teleza mara ukawa upo nyumbani ukala ugali na bamia ukashiba mara ukawa darasani na babu yako mzaa babu mara ukafa yaani ilimradi tu)
 
Mkuu umesema leo tena umeota, kwani uliwahi ota ndoto inayofanana na hiii?
 
Wazazi watakufa, mtakosana na dogo.

Bibi ndo ziraeli, yawezekana kipo kitu mzazi wako hakumfanyia bibi yaani mzazi wake.

Sala na dua zaweza badilisha mabaya yakawa mema. Usipofanya hivyo huyo bibi haondoki bila roho za watu,

Ni hivyo tu lakini.
 
Ondoka hapo ukapange utakufa siku si zako
 
Acha kutisha watu
Wazazi watakufa, mtakosana na dogo.

Bibi ndo ziraeli, yawezekana kipo kitu mzazi wako hakumfanyia bibi yaani mzazi wake.

Sala na dua zaweza badilisha mabaya yakawa mema. Usipofanya hivyo huyo bibi haondoki bila roho za watu,

Ni hivyo tu lakini.
 
Back
Top Bottom