Kuna nyakati Malaika wa kheri nao hutembelea motoni

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
Ayo si maneno yangu ila yao ni maneno ya FARID KUBANDA maarufu kama FID Q kwenye nyimbo yake ya BONGO HIP HOP.

kwa haraka haraka ayo maneno unaweza ukayachukulia kawaida tu ila aya maneno tunaishi nayo kwenye maisha yetu ya kila siku.

TWENDE KWENYE HISTORIA KIDOGO

Tarehe 24 mwezi wa 6 Mwaka 1947. Bondia RAY ROBINSON alimpiga bondia JIMMY DOYLE. lakini kabla ya pambano hilo RAY ROBINSON alitaka kualisha ma
pambano kwani alikuwa na hofu na ndoto aliyoota. kuwa kwenye pambano hilo angeenda kupigaja na JIMMY basi angemuua lakini alipembelezwa akaingia uwanjani ndoto yake ikawa kweli. RAY akampiga mpinzani wake JIMMY na kupelekea kifo cha JIMMY.

KUNA JAMBO LA KUJIFUNZA KWA KARIM MANDONGA.

Tucheke weeeh ila tukimaliza kucheka nina swali naomba niwaulize hivi munalikumbuka lile jina la yule bondia laiyempiga KARIM MANDONGA round ya 1 .

najua wapwa hamumkumbuki jamaa naitwa nani [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

ila pia hata kama mtu akionesha picha ya SHABAN KAONEKA pia itakuwa ngumu kumjua kama huyu ndo alimpiga KARIM MANDONGA ... TKO ROUND ya 4.

na mungu mwenyewe kamuumba binadamu na kumuweka dunia sio kwa lengo aje kukaa tu . lengo moja wapo la kuletwa duniani.

Ni kuchallenge kiakili mara nyingi upimwa uwezo wake kwa matatizo na mara chache upimwa kwa furaha ambayo furaha hiyo hiyo inaweza ikazalisha tatizo tena kubwa tu.

leo hii unajikuta hauna familiy unawaza kuoa hapo inakuwa umesolve tatizo moja kuwa umeshapata mwenza wako ila ushatengeneza tatizo jingine kuwa huyo mwenza wako anaitaji huduma sasa kama mwanzo ulikuwa haujishuhurishi sana sasa hivi unatakiwa upambane ili kupata kipato kwa ajili yako na mwenza wako.

Unaweza ukawa upo ndani ya ndoa lakini hauna mtoto ukipata mtoto unakuwa umeshawin sehemu moja lakini ushatengeneza tatizo jingine. kuna fundi wangu moja alipowahi kuulizwa kati ya pesa na mtoto kipi unakitaka upewe na kipi sio mbaya kama ukikikosa alijibu...

" NATAKA PESA BORA NIKOSE MTOTO MAANA PESA HAIWEZI KUMPIGA MTU ILA MTOTO ANAWEZA AKAENDA KUVUNJA KIOO CHA WATU CHA GARI IKAITAJIKA PESA AMBAYO SINA"..

Na kuna wakati matatizo uja kwa malengo tofauti kuna mda yanakuja kwa lengo la

1. Kukufikisha mahala fulani

2. Kukuonesha watu sahihi kwenye maisha yako wa kuwa nao

3. Kuwaondoa watu fulani kwenye maisha yako

KARIM MANDOGA yupo tofauti na mabondia wengine kama HASSAN MWAKINYO, COSMAS CHEKA , TWAHA KIDUKU na DULLA MBABE.

Baada ya mapambano wake ule aliopigwa round ya kwanza. sikutegemee kama kuna kitu chochote kingeendelea kwa MANDONGA lakini imekuwa tofauti kabisa .

kivipi [emoji848].

DULLA MBABE bingwa la maneno mtoto wa kizaramu alipopigwa alipakwa kejeri tu kuwa aachane na ngumi. ikafikia hatua mpaka akawaomba samahani mashabiki zake kwa kuwaangusha kwa round ya pili mfululizo . kimya kimetawala mpaka dakika hii

Lakini MANDONGA yeye kawa trending tokea alivyopoteza pambano lake la kwanza . media kubwa kubwa ikiwepo CLOUDS FM ilimuongelea sana na MANDOGA nae akajua kutembea na kitonga akasema kaanzisha vita na Watangazaji wa CLOUDS FM kipindi cha LEO TENA.

Baada ya mda mfupi MANDONGA huyo huyo akapata shavu la kusaini mkataba mkubwa tu jina la kampuni limenitoka ila mkataba ulikuwa unahusiana na mambo ya ulinzi.

Sasa hapo juzi kabla ya pambano lake yeye na shabani kaoneka kama tungekuwa na mjumuisho wa post zote zilizolike , comments , views basi nadhani KARIM MANDONGA angepata ushindi wa kufatiliwa zaidi kuliko hata ERICK KATOMPA na SELEMAN KIDUNDA .

Hii katika maisha ya kawaisa inatufunza kuwa kila mtu ana riziki yake. na mungu akitaka kukufungulia sio lazima akupe kwa njia ambayo itakupendeza ndo pale tunapoambiwa

" UKIPATA SHUKURU UKIKOSA USIKUFURU".

Ila kwa upande wa mchezo wa boxer hii sio swala zuri hata kidogo. na ikiwezekana lisijirudie mara kwa mara uwezo wa mabondia kama mandonga naweza kusema hatuiitaji .

inakuwa fedheha kubwa sana tukimpeleka bondia nje ya nchi alafu akipigwa TKO round ya 1.

Chama kinachosimamia mchezo wa ngumi. kinatakiwa kikae chini. na kuweke mipango kazi ya kuendeleza mchezo wa ngumi pamoja na kuboresha maisha ya mabondia inakuwa ajabu sana bondia anapigana tarehe 29 march 2022 alafu tarehe 30 jul 2022 baada ya miezi 3 tu unamuona tena ulingoni.

Hii inaonesha kama mabondia wanapigana njaa inawezekana mapato kidogo wanayoyapata baada ya mpambano ni kidogo inapelekea bondia kurudi uwanjani kutengeneza pesa huku akisahau Career yake inaweza ikaalibika na ikamkoseshe vitu baadae.

RESPECT HASSAN MWAKINYO KWA KUJUA UNACHOKIFANYA.

Muandishi: Ally nassor px

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…