Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Hichi ulichoongea nacho kina ukweli.

Binafsi huwa nikiangalia dunia na mifumo yake huwa nashindwa kuelewa kwanini binadamu tuna akili kuliko wanyama ila hazitusaidii kuwa tofauti na wanyama linapokuja suala la mfumo wa kutuwezesha kufahamu maisha ni nini.

Tumejiwekea mipaka na matabaka ya kufikiri kwa jina la uchumi, tukajibana kimaeneo na kuyapa majina kuwa hii ni nchi na tukabuni mtindo wa kuishi tukauita siasa na kutengenezea mifumo ya ulinzi dhidi ya binadamu.

 
Natamani ningekuwa na uwezo wakuishi miaka 1000 ijayo nione mabadiliko ya uelewa wa binadamu katika nyanja zote na je mazingira yanayomzunguka binadamu yatambadilikia au lah!, ila ni ngumu sana kwa hilo kuwezekana kwasasa! maana mfumo wa ulimwengu kwa viumbe hai si kuishi milele ila ni kuishi kwa kutoa new offspring huku ukitumia past ya viumbe waliopita ku adapt mazingira!..
Ni sawa na uweze kumfufua mtu alieishi mika 1000 iliyopita umlete sasahivi ni aidha anaweza kufa haraka sana maana huenda akakutana na magonjwa makali japo kwetu sisi yakawa ya kawaida ambayo gene yake haijamuwekea kinga!, au uwezo wake wa akili ukashindwa ku survive kutokana na mambo mengi kubadilika mno kuanzia matumizi ya technology, tiba, vyakula n.k

Binafsi sidhani kama kuna limit juu ya uwezo wetu na ulimwengu ila ninachokiona ni kuwa tunaenenda taratibu tu, ulimwengu hauna shida ya kutufunulia elimu na ujuzi swala lipo ni kuutumia hapo ndipo inapoweza kuwa tabu na ikitokea tukawa na maarifa yote basi jua ustaarabu nao utakuwa wa hali ya juu!.
hebu fikiri binadamu akija kuweza kuichezea space na kuiharibu!, sasa akifikia hayo maarifa hata ustaarabu wake hautakuwa wakawaida maana hilo ni bomu kushinda hata la nyuklia...😅
 
Mabadiliko makubwa yatakuja kutokea siku tukipata janga kubwa la moja kwa moja ambalo litatishia uhai wetu kutokana na life style yetu!. ila bila hivyo hakuna badiliko utaona kwasasa!.
 
Natamani ningekuwa na uwezo wakuishi miaka 1000 ijayo
Hichi ndicho nilichosema hapo nyuma kuwa binadamu akifahamu namna ya kudhibiti kifo mambo mengi yatagundulika. Imagine wewe, Mtanzania ambaye hujafanya ugunduzi wowote unayo hii curioisty, vipi kwa zile big brains zilizogundua kuwa dunia ni duara na kuna space? Leo zingekuwa na mtazamo upi iwapo zingekuwa hai?
 
Mabadiliko makubwa yatakuja kutokea siku tukipata janga kubwa la moja kwa moja ambalo litatishia uhai wetu kutokana na life style yetu!. ila bila hivyo hakuna badiliko utaona kwasasa!.
Kweli mkuu, hata ikitokea tukapata tishio la viumbe hai kutoka sayari nyingine mambo mengi yanaweza kubadilika.
 
Kuna swali moja Brian cox aliuliza, je hivi kama binadamu akiendelea zaadi akawa na elimu ya kila kitu, je hii itaondoa sifa yake ya kuwa mwanadamu maana sifa ya mwanadamu ni kuwa na curiosty ya kujua vitu, hivyo kama akishajua kila kitu anakuwa bored na maisha
 
Haha! hii huwa inanifanya niwaze kuwa sisi ni mashine na curiosity ni kitu kinachotufanya tuendelee kufanya kazi ili kile kinachofaidika nasisi kiendelee kufaidika tu!. ni mawazo tu!.
Binadamu hata akifikia hitimisho huenda bado kukawa na namna ikamfanya aendelee kupenda kuishi naweza kusema ni kama kula ama kufanya tendo la ndoa nahisi inaweza kuwa hivyo lakini pia binadamu sio kiumbe mvivu mvivu binadamu ni mbunifu hakosi lakufanya...😂
 
Elon anawatengenezea cheap zitakazofanya kuishi milele😅😅😅.

What if ustaarabu kadri unavyokua ndivyo tunavyozidi kujikaanga wenyewe😅😅
 
Elon anawatengenezea cheap zitakazofanya kuishi milele😅😅😅.

What if ustaarabu kadri unavyokua ndivyo tunavyozidi kujikaanga wenyewe😅😅
Mh! ustaarabu hukuwa sambamba na elimu itakuwa tabu elimu ikikuwa halafu ustaarabu ni sifuri hapo shida ndo itakuwepo na ukishakuwa na elimu basi ustaarabu muhimu alasivyo itakuwa haina maana ya elimu kama hakuna ustaarabu!..
 
Kwa hyo unahisi kila binadamu anavyopata elimu ubongo unaongezeka nguvu hivyo anabuni mbinu nyingi za kufanya kitu, kwa mantiki hyo unasema elimu haina mwisho kabisa au tutafanya cycle ya elimu kwamba wakishajua kila aina ya kufanya kitu wataanza kurudia mbinu za kale kwa wale wasiojua, mfano dunia ya Ai ikizidi itafanya watu wakumbuke Analog na itaendelea hivyo hivyo pia
 
Anaweza asirudie vya zamani anaweza akabuni mambo makubwa zaidi maisha ni sayansi na ni sanaa pia!, hizi ni fikra zangu tu sijui ulimwengu utampa nini binadamu kama akifikia hatima ya maarifa so hazi bado ni nadharia tu!
 
Kwenye sayansi hakuna tatizo lolote kusema "SIJUI/HATUJUI/BADO HAIJULIKANI"
Kabisa hicho ndio nachopenda kuhusu sayansi ila sayansi inaweza kuwa na unafiki pia, mfano wanasema kuna energy ambayo hawawezi kuiona wala kuipima ila wanajua ipo na wakaipa na jina la dark energy wanasema ilikuwepo kabla hata ya big bang ila ukiangalia hizo sifa ukisema hyo energy inaweza kuwa ndio creator wanasema hakuna kitu, Ironic si ndio😅
 
Kwa sababu sayansi haina uelewa na maelezo ya kutosha kuhusu dark energy huo sio uthibitisho wa dark energy kuwa creator, Sayansi huita mtazamo wako kama fallacy ya "God of the gaps".
 
Kwa sababu sayansi haina uelewa na maelezo ya kutosha kuhusu dark energy huo sio uthibitisho wa dark energy kuwa creator, Sayansi huita mtazamo wako "God of the gaps".
Nakubali hawana uelewa wa kina kuhusu dark energy ila hawajotoa possibility ya uwepo wake, wapo nusu nusu kwamba inaweza kuwepo au isiwepo ila kwa nini kwenye Creator hawaachi possibility kwamba huenda kukawa na nguvu inayohusika na ulimwengu, sisemi mambo wanayosema kwenye dini amna nasema ile nguvu ambavyo inahusika na ulimwengu
 
Hawajaondoa possibility ya dark energy kwa sababu wanaona ulimwengu unatanuka na kwa mifumo ya kisayansi ili kitu kitanuke kinahitaji nishati ya kusukuma au kuvuta, kwa upande wa muumbaji wanaona ukikubali muumbaji yupo linazuka swali lingine lisiloisha la nani kamuumba huyo muumbaji unayemuamini wewe.
 
Mawazo yako yanakwambia mungu amekaa sehemu, amekaa huko mbinguni .. Mungu ni imagination character tu, ambae amekuwa programmed kutoka kwa watu walio kumezesha.
Usi picture mungu wa kwenye vitabu vya dini, picture energy illiyoanzisha ulimwengu, siyo lazima kitu kiwe na characteristics za kiumbe ndio kiwe conscious kama particle zinauwezo wa ku behave tofauti kwa nini kusiwe na energy inayoweza ku behave tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…