Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Mwaka jana mgogoro kati ya serikali na wafanyabiashara ulikuwa mkubwa kiasi cha kumtoa Waziri mkuu ofisini na kuja kusuluhisha. Pamoja na waziri wa fedha Mwigulu kutupiwa lawama zote kwenye mkutano ule alitoa ahadi kadhaa za utatuzi mbele ya waziri mkuu.
Ajabu, kama asemavyo CG wa TRA ni kuwa hakuna muswaada wowote uliopelekwa Bungeni kubadili sheria hizo hivyo TRA kwa vile inafanya kazi kwa mujibu wa sheria lazima watekeleze.
Hiki ni kiburi cha Mwigulu kwani ni kama vile mamlaka ya uteuzi inamuogopa au KESHA IWEKA MFUKONI kama alivyoiweka ile timu mashuhuri ya mpira.
Ni hasara ngapi amezisababisha kwa ujeuri anaofanya na haondolewi hapo?
Mjue kila jambo baya litokeapo kwenye nchi huwa lina chanzo chake, na madhara ya mgogoro huu wa kibiashara yatakuja kutupeleka pabaya au mnataka watu watoroke maofisini kwa Ambulance kama Kenya?
Mwigulu kamfanya nini mteuzi hadi ana mhofia?