Kuna Picha Kuwa Mamlaka Inamuhofia Mwigulu Ndio Chanzo cha Migogoro Kuwa Endelevu

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Mwaka jana mgogoro kati ya serikali na wafanyabiashara ulikuwa mkubwa kiasi cha kumtoa Waziri mkuu ofisini na kuja kusuluhisha. Pamoja na waziri wa fedha Mwigulu kutupiwa lawama zote kwenye mkutano ule alitoa ahadi kadhaa za utatuzi mbele ya waziri mkuu.
Ajabu, kama asemavyo CG wa TRA ni kuwa hakuna muswaada wowote uliopelekwa Bungeni kubadili sheria hizo hivyo TRA kwa vile inafanya kazi kwa mujibu wa sheria lazima watekeleze.
Hiki ni kiburi cha Mwigulu kwani ni kama vile mamlaka ya uteuzi inamuogopa au KESHA IWEKA MFUKONI kama alivyoiweka ile timu mashuhuri ya mpira.
Ni hasara ngapi amezisababisha kwa ujeuri anaofanya na haondolewi hapo?
Mjue kila jambo baya litokeapo kwenye nchi huwa lina chanzo chake, na madhara ya mgogoro huu wa kibiashara yatakuja kutupeleka pabaya au mnataka watu watoroke maofisini kwa Ambulance kama Kenya?
Mwigulu kamfanya nini mteuzi hadi ana mhofia?
 
Mwigulu Ana kiburi sana
Labda Yale yaliyotokea Kenya yatokee na hapa pia yawanyooshe wawajeshimu wananchi
 
We kwenye issue serious unaleta masikhara

Akili yako siyo nzuri
Magufuli, Lowasa na Mwigullu walibarikiwa na Nabii na Mtume TB Joshua

Kama hutaki hizo ni Chuki binafsi sina Cha kukusaidia ๐Ÿผ๐Ÿ˜‚
 
Acha character assassination kwa Mh. Mwigulu....heshima ni kitu cha bure
 
Magufuli, Lowasa na Mwigullu walibarikiwa na Nabii na Mtume TB Joshua

Kama hutaki hizo ni Chuki binafsi sina Cha kukusaidia ๐Ÿผ๐Ÿ˜‚
Unamaanisha naye ataungana na wenzie hivi karibuni?
 
Ni kweli kabis . tatizo ni Mwigulu, na kwa vile kawaweka wakubwa mfukoni anafanya kama anavyotaka.
 
Sasa kama anaempa jeuri ni chura kiziwi unadhani watu wataongea nini ili aelewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ