Kuna Propaganda Zinaendelea dhidi ya Matokeo CSEE 2012

STEIN

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Posts
1,771
Reaction score
553
Ndugu wanaJF,

Kuna watu wamepewa hela na kuzunguka kwenye Vijiwe na kwenye Daladala Kazi yao kubwa imekuwa ni kuwaponda Waalimu na Wanafunzi kwenye swala hili la Matokeo ya form four kuwa mabaya sana Mwaka huu.

Tangu Mwishoni mwa Wiki iliyopita mimi binafsi nimeshuhudia mara nyingu Swala hili likijadiliwa katika mrengo wa kuwakatisha tamaa Waalimu na Wanafunzi kana kwamba waalimu ndiyo waliowafelisha wanafunzi moja kwa moja.

Watu hao wameenda Mbali zaidi na kufika Mahali eti Wanafunzi wa siku hizi hawana akili ndiyo maana wanafeli maana uwezo ni dhaifu.


Kwa analysis niliyofanya watu hawa hata uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo kiasi kwamba hata factors zinazochangia Ufeli na Ufaulu wa Mtahiniwa wao hawazijui ukiwa Chalenge kidogo tu utasikia huyu ni CHADEMA nini!!!!


My Take hivi tutafanya Propaganda hizi hadi lini?

Leo hii Madaktari wakigoma, Waalimu wakigoma, Wanafunzi wakifeli tunatoa hoja nyepesi.
 
Vijana wa lumumba kwa kina nape hao!
 
Hizo hela za bure ziko wapi jamanai, hapa kwetu pamekauka ile mbaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…