Ndugu wana jamvi kuna sababu ya kujua mpenzi wako unayetaka kumuandaa kuwa my wife au my husband alikuwa anaishije kwenye maisha yake ya kimapenzi hapo nyuma. Tusaidiane maana nataka kuingia katika maisha ya ndoa lakini bado sijampata wa kumoyo.
NB: Wana JF inawezekana hii thread ilishajadiliwa hapo nyuma lakini TAFADHALINI tusaidiane tena kimawazo wanajamii wenzangu!!
Kuna watu wengine wana wivu wa ajabu sana. Kama unataka mke au mume ambaye ni bikira 🙂 basi wapo kibao! we tangaza tu unataka bikira basi utapata maelfu ya watu kisha utafanya uchaguzi wako. Umchunguze mke/mume wako ili kujua katembea na watu wangapi ili iweje? halafu ukishajua itakusaidia nini? Bora ungesema woote mchunguze afya zenu ili kuhakikisha hamjangusa miwayawaya kabla ya kuingia kwenye ndoa yenu.
My dear Sipo, ni vizuri kufahamu hata kidogo back ground ya mpenzi wako, unaweza kujua back ground si kwa kwa kufahamu katembea na wangapi la hasha! Penda kujua familia yake ipoje. Kama ni watu wazuri na watakuwa na upendo na ww. Tabia zao zipoje ili usije na ww kupata watoto wenye tabia chafu kama wao ikiwa tabia zao mbaya.
Mie sioni umuhimu wa kujua mpenzi wako alitembea na nani, maana ya kale yamepita tazama sasa mmeanza mapya. Kama mwenyewe akijipendekeza kukwambia is ok, lkn sio kumhoji hoji mtu.