Sio kweli! Kinachotokea hapo ni kitu kidogo tu. Unapoweka full tank maana yake hata reserve chamber zinakuwa full. Jambo ambalo husababisha mafuta yanayotumika kufidiwa na yale ya reserve na hivyo kuifanya gage yako iendelee kusoma full...wewe hapo huona mafuta bado yamejaa, lkn inapotokea reserve imetumika, yale mafuta yanayoratibiwa na kipimo chako huanza kutumika na hapo utaanza kuona mshale unasoma kama kawaida..
Nijuavyo Mimi ni kwamba trip za hapa na pale hutumia mafuta mengi kuliko trip ndefu ama long safari, hii hasa ni kwa magari ya petrol. Sababu kubwa ni mfumo wa uchomaji wa mafuta.. Gari za petrol zina mfumo ambao ili mafuta yaingie kwenye mzunguko, ni lazima kwanza yachomwe! Sasa pale mafuta yanapokuwa yameunguzwa tayari kuingia kwenye mzunguko na wewe ukazima gari, maana yake ni kwamba mafuta hayo yatakuwa hayana kazi pindi utakapowasha tena gari kwani yatahitajika mafuta mapya yachomwe ili kuendelea na mzunguko!
Hii ni sababu ya wazi kitaalamu. Hata hivyo, zipo sababu nyingi zinazochangia mabadiliko ya ulaji wa mafuta kwenye gari, mfano njia unayopita, uzima wa gari lako na vipuri vyake, aina ya uendeshaji n.k.