Kuna sehemu viongozi wa Yanga walikosea

Kuna sehemu viongozi wa Yanga walikosea

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
Sipo hapa kulalamika na wala sio kawaida yangu kuandika uzi wa kulalamika, binafsi matokeo ya leo hayawezi nifanya kukata tamaa kwani naijua football vizuri, bado timu ina nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano yote inayoshiriki.

Wala sitaki kupeleka lawama zangu kwa kocha huyu mpya kwani bado ni mapema sana kumuhukumu, ila lawama zote wanastaili viongozi maamuzi ya kumtimua GAMOND yalikua ya kukurupuka sana, binafsi naona kabisa hii game ilikua nyepesi sana kwa master GAMOND.

Soma Pia: FT: Young Africans SC 0 - 2 Al Hilal | CAF CL | Benjamin Mkapa Stadium | 26.11.2024 |

Poleni sana wananchi wenzangu hiyo ndio football.
 
Umeongea ukweli mtupu, na kitu kingine inaonekana baadhi ya wachezaji wa yanga kama Azizi kiy viwango vimeshuka sana, tatizo sijui ni nini? Au starehe
 
Kocha ameajiriwa ili afukuzwe, kama hafanyi vizuri na afukuzwe tu aje mwengine
 
Kotokuheshimu professional za watu na ujuaji wa kipumbavu ndiyo unaoua maendeleo ya soka bongo🚮🚮
Yanga haijawahi kuwa na heshima, walimsajiri Dube kama sehemu ya kuwakomoa Azam. Yanga Hawa Hawa walikomaa na Faisal kisa ugomvi wa ndani ili hali soka ni biashara. Yanga wanaendesha timu kipumbavu sana.
 
Haswaaaa, waswahili wana ujuaji fulani kujikuta wao ni wataalamu kuliko wataalam wenyewe, matokeo huwa yanaonekana
 
yule coach alisema kuwadunga kitu wachezaji ingewaharibu sana. akaonekana mbaya na ndo kitu tunachokiona kwa sasa wachezaji hawana uwezo bila kudungwa
 
Sipo hapa kulalamika na wala sio kawaida yangu kuandika uzi wa kulalamika, binafsi matokeo ya leo hayawezi nifanya kukata tamaa kwani naijua football vizuri, bado timu ina nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano yote inayoshiriki.

Wala sitaki kupeleka lawama zangu kwa kocha huyu mpya kwani bado ni mapema sana kumuhukumu, ila lawama zote wanastaili viongozi maamuzi ya kumtimua GAMOND yalikua ya kukurupuka sana, binafsi naona kabisa hii game ilikua nyepesi sana kwa master GAMOND.

Soma Pia: FT: Young Africans SC 0 - 2 Al Hilal | CAF CL | Benjamin Mkapa Stadium | 26.11.2024 |

Poleni sana wananchi wenzangu hiyo ndio football.
Kuna changamoto ambayo ipo Yanga kuanzia kwa Gamond. Eneo la ushambuliaji limekuwa butu kupita maelezo sijui shida ni nini. Game kama ya leo ilikuwa ni game ya kushinda kabisa kwani Yanga walimiliki mpira kwa kiwango kikubwa, ila hawakuweza kutafuta nafasi nzuri za kufunga.
Pia kuna wakati Yanga wanakuwa slow kwenye mpira na back pass nyingi bila sababu za msingi.
Dube wampe muda arelax kwanza, Kibabage ni kimbia kimbia ila hana akili za mpira. Pia
 
yule coach alisema kuwadunga kitu wachezaji ingewaharibu sana. akaonekana mbaya na ndo kitu tunachokiona kwa sasa wachezaji hawana uwezo bila kudungwa
Hii hoja haina mashiko, Yanga wanacheza kwa nguvu ile ile, umaliziaji ndio unaisumbua Yanga na sio wachezaji kuchoka.
 
Sipo hapa kulalamika na wala sio kawaida yangu kuandika uzi wa kulalamika, binafsi matokeo ya leo hayawezi nifanya kukata tamaa kwani naijua football vizuri, bado timu ina nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano yote inayoshiriki.

Wala sitaki kupeleka lawama zangu kwa kocha huyu mpya kwani bado ni mapema sana kumuhukumu, ila lawama zote wanastaili viongozi maamuzi ya kumtimua GAMOND yalikua ya kukurupuka sana, binafsi naona kabisa hii game ilikua nyepesi sana kwa master GAMOND.

Soma Pia: FT: Young Africans SC 0 - 2 Al Hilal | CAF CL | Benjamin Mkapa Stadium | 26.11.2024 |

Poleni sana wananchi wenzangu hiyo ndio football.
Hisia ndizo zinaongoza club zetu,Singida nao wamekopi vilevile. Hisia zimemuondoa Gamondi,vilevile ndizo zimefanya tukahama uwanja. Sasa sijajua na leo tutahama uwanja........
 
Hapa mchawi ni Sindano, hii ndio Yanga halisi. Ole wenu mrudie sindano CAF wanawaona.
 
Yanga haijawahi kuwa na heshima, walimsajiri Dube kama sehemu ya kuwakomoa Azam. Yanga Hawa Hawa walikomaa na Faisal kisa ugomvi wa ndani ili hali soka ni biashara. Yanga wanaendesha timu kipumbavu sana.
Umesahau kila mwaka walikuwa wanamsajili Chama hatimae kwa hila zao wakamchukua
 
Umeongea ukweli mtupu, na kitu kingine inaonekana baadhi ya wachezaji wa yanga kama Azizi kiy viwango vimeshuka sana, tatizo sijui ni nini? Au starehe
🐒
1000016457.jpg
 
Yanga mbele imelegea nyuma imetoboka, ule mwiko nyuma umewatoboa
 
Back
Top Bottom