Kuna sheria inayozuia kufungua makanisa kila sehemu?

Kuna sheria inayozuia kufungua makanisa kila sehemu?

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
Samahanini wadau,

Kwa nitaowakwaza ila hili jambo la kufungua makanisa popote tu bila kujali location mfano jirani na ninapokaa wamefungua kanisa uani na wanaimba toka saa nane mchana na ibada mpaka sa 6 za usiku.

Majirani hatulali wala hatusikilizani. Nadhani sio jambo geni kila sehemu, kwenye magodown na viwanda vya zamani wanafungua.

Kwenye madarasa ya shule baada ya wanafunzi kutoka wanafungua nadhani imekua usumbufu jamani, uhuru wa kuabudu umeruka kikomo.

Kama kuna sheria kuhusu hilo jambo naomba nisaidiwe nimuhamishe huyu jirani.
 
Kama town plan inaonesha eneo hilo limetengwa kwa ajili nyumba za ibada hakuna tatizo. Kama ni eneo mahsusi kwa ajili ya makazi na kanisa limekuja baadae hilo ni kosa. Mnaweza kuji organise wakazi wa hapo mkapeleka malalamiko yenu serikali za mitaa kwa hatua zaidi huko Manispaa/mji na hatimaye kwa mwanasheria wa serikali. Hilo ni suala la madai la PUBLIC NUISANCE ambalo DPP pekee ndo mwenye mamlaka ya kufungua shtaka. Pia hili lipo kama jinai na madai pia. Hata hivyo ktk mazingira machache mtu binafsi ambaye anaathirika zaidi na kelele hizo kuliko wengine anaweza kufungua kesi ya madai mahakamani kuomba remedies mbalimbali kama fidia au amri ya kukataza shughuli za kanisa hilo kuendelea ktk eneo hilo.
 
Back
Top Bottom