Mapolomoko hicho ndicho nilichokielewa pia. I second you.
Mkuu ujenzi wa nyumba una masharti mengi.. Kwa kifupi ili ujenge nyumba inabidi upate kibali toka manispaa ya wilayani kwako baada ya wewe kuwasilisha michoro ya ramani ya nyumba yako iliyo na mhuri wa consultant firm inayotoa architectural services..
Vile vile ziko sheria za miji ambazo zinakulazimisha kuomba kibali manispaa unapotaka kubomoa nyumba au jengo.. Vile vile zinakulazimisha kuomba kibali manispaa unapotaka kuzungushia ukuta sehemu unayotaka kubomoa..
Kwa hiyo unapotaka kufanya marekebisho yeyote kwenye nyumba ambayo ina michoro iliopata kibali unapaswa kutoa taarifa manispaa..
Tatizo hapa ni nyumba nyingi hapa kwetu hazijajengwa kwa misingi hiyo.. Ikiwa ni pamoja na hiyo..
Na watendaji wa mitaa ndo wana-act kama enforcers wa sheria hizo.. Imegeuzwa miradi wa kujipatia fwedha..