Kuna sheria Tanzania ya mtu kuanza kifungo kabla hujahukumiwa ?

Kuna sheria Tanzania ya mtu kuanza kifungo kabla hujahukumiwa ?

Bowie

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
4,373
Reaction score
6,084
Leo kwenye Magereza yetu kuna akina Kitilya, Manji, Malinzi na mahabusu wengine wengi ambao kila wakifikishwa mahakamani wanaambiwa upelelezi unaendelea.

Kwanini mtu ama watu wakamatwe na kunyimwa dhamana wakati ushahidi haujakamilika.

Na kwanini wanyimwe dhamana. Serikali ya awamu ya 5 iangalie kwa makini suala kumyima mtu haki zake za msingi na kumweka mtu mahabusu kwa muda mrefu wakati mwisho anaambiwa hana kesi ya kujibu.

Rais Magufuli majuzi aliwaambia Takukuru wahakikishe wanawashughulikia watuhumiwa ambao kuna ushahidi kamili.
 
HAKUNA MTU ALIYE JUU YA SHERIA.... INABIDI TUISHI KWA KUFUATA SHERIA, BINAFSI ACHA WAKAE TU HUKO MAANA WANAMAKOSA

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatukatai hakuna mtu aliye juu ya sheria lakini mtu huwezi ukamweka rumande miaka miwili bila dhamana ukidai upelelezi unaendelea. Ukifanya hivyo utakuwa umemnyima haki zake za msingi.
 
Back
Top Bottom