Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zetu za uchaguzi zinataka mtu ukigombea nafasi yoyote ya kisiasa ni lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa na kinachotambulika.
Kwa msingi huu wa sheria ina maana ukipoteza unachama wako ina maana umepoteza pia sifa za uongozi wowote ulio nao ambazo msingi wake ni huo unanachama. Hapa naongelea Ubunge, Uwaziri na hadi Urais.
Kuna siku ambayo mtu tayari ni Rais wa JMT halafu ndani ya chama chake kukatokea mgogoro akafukuzwa au kusimamishwa unachama. Yatazuka maswali uhalali wake wa kuendelea kuwa Rais wa JMT.
Sikumbuki vizuri kisa cha wale Covid 19 wa CHADEMA kina Mdee na shoga zake kama walifukuzwa au kusimamishwa na chama ila ni case mojawapo ya mapungufu ya katiba na sheria tuliyonayo na jinsi ambavyo wakati mwingine tunaisigina katiba.
Tunaenda na haya mapungufu hivyo hivyo tu lakini kuna maeneo ambapo mkanganyiko ni mkubwa na kuna siku utakuwa mkubwa sana.