kipchog
Member
- Jun 24, 2024
- 21
- 27
Ndugu wanajamvi wenzangu mabibi na mabwana natumai mu wazima. Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, naomba kufahamu Kuna siri gani imejificha kwenye mwenge.
Wiki iliyopita kulikuwa na shamra shamra za mapokezi ya mwenge wa uhuru eneo nililopo. Sasa mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo katika mapokezi hayo.
Kulikuwa na shamra shamra za hapa na pale wakati tukiwa tunausubiri mwenge na nilikuwa nimevaa kofia(cape). Wakati huo kulikuwa na vijana wanaoimba imba na kufanya eneo lile liwe na uchangamfu.
Kama sijakosea nafikiri ni skaut. Chakushangaza wakati mwenge unapita katika eneo nililokuwepo akaja kiongozi wa vijana wa wale waliokuwa wanachamgamsha kwa kuimba akaniambia "geuza kofia" yaani ile sehemu ya mbele iende nyuma na sehemu ya nyuma iende mbele.
Nikatii agizo kwasababu najua wale watu hawanaga mbili. Ndugu wanajamvi wenzangu naomba kujua maana ya kitendo hicho ni Nini?
Lakini pia wale vijana waliokuwa wanaoimba walikuwa wanaimba matusi matusi tu. Ki ukweli sijasikia nyimbo za kizalendo au zenye maadili, mpaka nikajiuliza au huu mwenge una agenda ambazo zimejificha? Naomba mwenye ufahamu wa hili anijuze.
Ahsanteni.