Kuna siri nyuma ya pazia kwa Mo Dewji, baada ya kui-unfollow Simba, sasa ai-follow tena

Kuna siri nyuma ya pazia kwa Mo Dewji, baada ya kui-unfollow Simba, sasa ai-follow tena

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Siku chache zimepita tangu Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' alipoamua kuwa-unfollow wachezaji wote wa timu hiyo ambao alikuwa amewa-follow kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Jana, pia Mo ambaye ni Rais wa Heshima wa Simba aka-unfollow page ya klabu hiyo akibakisha ya Simba Queens ambayo aliipongeza kwa ushindi wao juzi wa mabao 7-0 dhidi ya JKT Queens.

Lakini saa kadhaa baadaye alibadili gia angani na kuamua kui-follow tena page ya Simba.

Haijajulikana sababu hasa iliyopo nyuma ya pazia ya Mo kufanya hivyo bila kuwa na ufafanuzi wowote.

Hivi karibuni ukurasa wake wa Twitter ulihusika kutoa tweet ambazo ziliwapa mashabiki na wadau wa soka hofu kwa kuwa hazikuwa zikieleweka hasa ujumbe wake wa moja kwa moja, aligusia suala la uwekezaji wake klabuni hapo, ambalo nalo limekuwa likizungumzwa mara kadhaa.

Chanzo kimoja kutoka ndani ya Klabu ya Simba kinaeleza kuwa inawezekana Mo anafanya hivyo kama sehemu ya mkakati wa kufanyika kwa jambo lingine ambalo hataki watu walizungumzie, kwa maana ya kubadili upepo.

Mo kwa sasa amekuwa mbali na klabu hiyo kwa kuwa alikabidhi cheo chake kwa Try Again ambaye pia amemfollow kwenye ukurasa wake Instagram.

Simba imekuwa na mwendo wa kusuasua tangu kuanza kwa msimu huu, kumekuwa na presha kubwa ya timu kutocheza vizuri na kutopata matokeo mazuri pia, huku upande wa pili uwekezaji wa Mo nao ukiwa bado mdomoni mwa wadau kujua mwisho wake upoje.
 
Na nyie mna m-follow sana MO, tafuteni mambo zingine mfanye, akigeuka kushoto utaskia MO ageukia kushoto, akirudi kulia MO sasa ageukia kulia, hiyo account ni yake wacha afanye atakavyo.
 
Na nyie mna m-follow sana MO, tafuteni mambo zingine mfanye, akigeuka kushoto utaskia MO ageukia kushoto, akirudi kulia MO sasa ageukia kulia, hiyo account ni yake wacha afanye atakavyo.

Simba haina pesa wala thamani in kanjibai voice.
 
Back
Top Bottom