Kuna Taasisi za Serikali hazifanyi vile ambavyo inapaswa

Kuna Taasisi za Serikali hazifanyi vile ambavyo inapaswa

chinatown

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
1,232
Reaction score
1,105
Kuna makundi hayatumiki sawa sawa katika nchi yetu*

Nimekuwa najitafakalisha juu ya makundi na taasisi za serikali kadhaa kama kweli zinashiriki kikamilifu kuijenga nchi nikagundua kuna sehemu hatufanyi sawa.

Kati ya taasisi za serikali ambazo hazitumiki ki weledi au kimkakati ni pamoja na Jeshi la wananchi Tanzania, na magereza(wafungwa) .

Nimekuwa nikiona jeshi la wananchi ambao kazi yao kubwa ni kulinda nchi mipaka yake ikijishughulisha na miradi mingine ya maendeleo kwa ajiri yao, miradi hiyo ni biashara ya vitu ambavyo tayari mtu yoyote anaweza kufanya.JWTZ wana biashara za maduka ya dawa, supermarkets, maduka ya pembejeo, kumbi za sherehe, yard za magari na car wash.

Najiuliza kwa nini taasisi kama hii isijikite kwenye uzalishaji wa vitu kama chakula, mali ghafi au utengenezaji wa vitu vyetu kama vile mwanzo uundaji wa magari yetu ya Nyumbu?

Kwa nini jeshi kama jeshi nao wafanye biashara ya vitu tunavyoagiza nje? Haya ni matumizi mabaya ya taasisi , haya nimatumizi mabaya ya rasilimali watu.Tunakumbwa na uhaba wa chakula kwa sababu serikali imewaachia watu wachache (wakulima wadogo wadogo) kuzalisha chakula nchini.Makundi haya yaani Jwtz na wafungwa wangetumika kwenye uzalishaji wa vitu kama chakula na mazao yatokanayo na ufugaji sidhani kama nchi yetu ingekuwa inapata uhaba wa chakula.

Sidhani kama tunahitaji kuwa na magereza mjini , sidhani kama jeshi letu liwe lina maduka ya pharmacy.Hawa wafungungwa kama wangetengenezewa mashamba makubwa na wakajikita kwenye uzalishaji wa chakula na mazao ya mifugo nadhani nchi ingekuwa na hifadhi kubwa ya chakula na tusingekuwa na haja ya kuagiza chakula nje ya nchi

Tuna mifugo ya kutosha katika nchi yetu .Tuna mifugo ya kila aina ni jukumu la serikali kuamua gereza fulani litafuga mifugo, na pia gereza fulani litalima mazao haya na haya, na hii itapunguza kama sio kuondoa kabisa jukumu la serikali kuwa na bajeti ndefu kuwahudumia wafungwa.

Hima sasa viongozi wa serikali mliopata dhamana ya kusimamia taasisi hizi badilisheni mtazamo kiutendaji ili kuisaidia nchi kusonga mbele

Badala ya kufikiria kuuza vitu vilivyo tengenezwa tayari muanze uzalishaji wa vitu /chakula kwa ajili ya watanzania wote.
 
Sawa mwanangu Asante Kwa ushaurii
FB_IMG_1724330690583.jpg
 
Back
Top Bottom