Tetesi: Kuna tafakari inafanyika kutaka ofisi za madehebu ya dini kuwa na picha ya Rais

Tetesi: Kuna tafakari inafanyika kutaka ofisi za madehebu ya dini kuwa na picha ya Rais

Tang Zhou

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2018
Posts
1,206
Reaction score
2,588
Mambo kama haya najua hupigwa chini haraka sana hapa JF maana pia tunafanya biashara...lkn wacha nifikishe tu ujumbe maana mjumbe hauawi...mambo mengine yanayoendela chinichini yanaogofya mno..

Nilikuwa nazungumza na Kiongozi wangu mmoja wa Kiroho leo amenieleza jambo ambalo limeniacha mwili wote ukiwa umelowa jasho na kutetemeka kwa woga...

Kwamba katika kikao kimoja walichoitwa na mmoja wa Wakuu wa Mikoa wa JPM, Mkuu huyo wa Mkoa bila chembe ya woga aliwaomba wamwunge mkono Rais Magufuli kwa kauli na matendo kupitia mahubiri na kuchangia miradi ya serikali...lakini kama hilo hawaliwezi, basi Waning'inize japo PICHA YA RAIS kwenye Ofisi zao kama ilivyo katika ofisi za serikali na makampuni binafsi maana kwa hakika Rais Magufuli ni chaguo la Mungu..

Mchungaji wangu anasema alitetemeka sana na kulia machozi maana anasema hiyo kauli inaonekana haikutolewa kwa bahati mbaya bali ni jambo ambalo inaonekana limejadaliwa kwa kina kama si ndani ya serikali basi ni ndani ya vikao vya CCM...angalau katika ngazi ya watawala hapa mkoani..

Mchungaji wangu anasema kumekuwa pia na udhibiti usio wa kawaida wa kazi za kiroho, ikiwemo kuratibiwa kwa mahubiri katika baadhi ya Makanisa na misikiti "korofi" pamoja na misaada wanayopokea kutoka kwa wafadhili wa nje.

Hakika Kama hautoshi uchokozi kwa Mungu ambao tayari umekwishakufanywa na watawala wa sasa, hii ni hatua yao nyingine kutaka kujenga Mnara wa Babeli kumfikia Mungu...HAWA WATAWALA WANA UJASIRI WA AJABU!
 
Kwani sasa picha hamna?? Kwann hamna?? Na ikiwepo nn tafsiri yake??
 
Nguvu nyingi zinatumika huyu kiumbe apendwe na wananchi, lakini kutwa anatoa maneno ya kejeli kwa wananchi.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Makanisa ya Kakobe yameweka picha zake. Ya Mwingira yote yamening’iniza picha zake. Hii tetesi sidhani kama itapokelewa vyema na viongozi wa dini.
 
Nyie bado hamjui Kama Magufuli ni chaguo la Mungu?
 
Mi nadhani watu wa karibu na mkubwa ndio wanaofanya mambo tofauti.

Hata wakati wa A 4 tulikua tunaambiwa kuwa mh. Mkubwa ana nia njema lakini watendaji wake ndio wanamharibia.

Ukishakuwa Mkubwa hata ukitawala awamu moja ni poa tu. Tena unapata Muda mzuri wa kula pension yako na heshima kibao. Huguswi na mtu yeyote. Kimyaaaa.
Tatizo ni wapambe ndio wanatamani Mkubwa atawale milele mana wanajua wengi wamepata vyeo kama zali la mentali.
 
hizo ni tetesi tu maana hata mimi nilikutana na kiongozi fulani akaniambia Mrema amewaomba wabandike picha za Mbowe lkn walimwambia wataziweka lkn ili zipendeze vizuri zinahitaji mwenyekiti avae miwani. Mrema alikataa
 
Mambo kama haya najua hupigwa chini haraka sana hapa JF maana pia tunafanya biashara...lkn wacha nifikishe tu ujumbe maana mjumbe hauawi...mambo mengine yanayoendela chinichini yanaogofya mno..

Nilikuwa nazungumza na Kiongozi wangu mmoja wa Kiroho leo amenieleza jambo ambalo limeniacha mwili wote ukiwa umelowa jasho na kutetemeka kwa woga...

Kwamba katika kikao kimoja walichoitwa na mmoja wa Wakuu wa Mikoa wa JPM, Mkuu huyo wa Mkoa bila chembe ya woga aliwaomba wamwunge mkono Rais Magufuli kwa kauli na matendo kupitia mahubiri na kuchangia miradi ya serikali...lakini kama hilo hawaliwezi, basi Waning'inize japo PICHA YA RAIS kwenye Ofisi zao kama ilivyo katika ofisi za serikali na makampuni binafsi maana kwa hakika Rais Magufuli ni chaguo la Mungu...Mchungaji wangu anasema alitetemeka sana na kulia machozi maana anasema hiyo kauli inaonekana haikutolewa kwa bahati mbaya bali ni jambo ambalo inaonekana limejadaliwa kwa kina kama si ndani ya serikali basi ni ndani ya vikao vya CCM...angalau katika ngazi ya watawala hapa mkoani..

Mchungaji wangu anasema kumekuwa pia na udhibiti usio wa kawaida wa kazi za kiroho, ikiwemo kuratibiwa kwa mahubiri katika baadhi ya Makanisa na misikiti "korofi" pamoja na misaada wanayopokea kutoka kwa wafadhili wa nje.

Hakika Kama hautoshi uchokozi kwa Mungu ambao tayari umekwishakufanywa na watawala wa sasa, hii ni hatua yao nyingine kutaka kujenga Mnara wa Babeli kumfikia Mungu...HAWA WATAWALA WANA UJASIRI WA AJABU![/QUOT

IWEJE PICHA YA SHETANI IWEKWE KWENYE NYUMBA ZA IBADA?
 
hizo ni tetesi tu maana hata mimi nilikutana na kiongozi fulani akaniambia Mrema amewaomba wabandike picha za Mbowe lkn walimwambia wataziweka lkn ili zipendeze vizuri zinahitaji mwenyekiti avae miwani. Mrema alikataa
Idiot
 
Back
Top Bottom