Habari za leo ndugu zangu.
Leo nimeona nije kupata ushauri kuhusu matumizi ya feni. Kila mara ninapolala usiku huwa natumia feni hiii ni kwa sababu ya hali ya joto la Dar Es Salaam ila ninasikia tetesi kuwa kuna matatizo kwa kutumia feni mara kwa mara nami nimekua na hofu kwa kua ninatumia feni kwa zaidi ya miaka mitatu sasa
Sasa naomba ushauri wa kitaalamu kuhusu jambo hili je inasababisha matatizo ya kifua? tafadhali mwenye ushauri anisaidie na kama kuna matibabu ambayo naweza kuyapata kabla matatizo hayajawa makubwa.
Asanteni sana