Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,205
- 5,121
Kwanza kabisa naomba niseme sijaripoti kwenye mamlaka zinazohusika sababu hawatalichukulia kwa uzito ama watachelewa kupata data tofauti na nikipost kwenye social media platforms kama hii data zitapatikana kwa urahisi zaidi na wahusika watalichukulia kwa uzito.
Kuanzia mwezi wa nne mwishoni nimekutana na wanawake kadhaa ambao wanalalamika wanatokwa na damu zisizokata baada ya kupata siku zao. Wengine wameingia kwenye siku zao tarehe ambazo sio tarajiwa, lakini nao wameendelea kupata bleeding isiyokata.
Kuna wanawake wengine wawili ambao walikuwa na mimba changa, nao wamepatwa na hili tatizo, mmoja alienda hospitali wakamwambia mimba imeshaharibika, mwingine alienda hospitali baada ya kupata bleeding non-stop kwa siku 7 lakini bahati nzuri mimba ikawa haijaharibika. Wote hawa walikuwa na mimba changa za chini ya miezi 2 ambapo hata kliniki hawajaanza.
Huko mahospitalini pia kuna cases kadhaa za namna hii, ambazo zina ufanano uleule wa kubleed non stop, wengine mimba zinakuwa zimeshaharibika, wengine Mungu saidia zinakuwa ziko salama.
Hii ni observation yangu kwa mkoa wa Dar sijajua mikoa mingine hali ikoje. Kwa vyovyote vile kuna kitu hakiko sawa na kinahitaji thorough investigations.
Wahusika kazi kwenu.