Kuna tatizo lisilojulikana Simba. Hata umlete Vinicius Jr, timu utaiona kama Namungo tu

Kuna tatizo lisilojulikana Simba. Hata umlete Vinicius Jr, timu utaiona kama Namungo tu

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Ninajua wapo wengi wanaowaza kama mimi. Kuna tatizo pale Simba halijapatiwa ufumbuzi.Wachezaji kucheza chini ya kiwango,kutojitoa ama kuumia wakati muhimu wakihitajika sana na timu.

Tumeona timu ikisajili wachezaji ambao wamekuwa bora sana walikotoka,lakini wakishakanyaga Simba tu, wanakuwa wachezaji wa kawaida sana hata timu ndogo haziwatamani.

Kuna propaganda kutoka upande wa pili zikihanikizwa na mashabiki wajinga wa simba kwamba Bocco alikuwa akiwapiga misumari wachezaji. Leo Bocco hayupo hali bado ni ile ile.

Kwa sasa wameanza tena kumshambulia Matola.Bila hata aibu hawana kumbukumbu kuwa Matola aliwahi kuondoka lakini timu ilifanya vibaya sana tu.

Ninashawishika kuamini kuwa kuna kitu ambacho tusipokigundua,hata tukisajili mchezaji wa kiwango cha dunia,hatafanya kitu zaidi ya kubeba lawama tu.

Upande wa pili wanaonekana kuwa wana siri za mambo haya.Mchezaji yeyote hata akionekana mbovu timu nyingine,akihamia kwao tu,ghafla anakiwasha sana na kuwa star.Hapa kuna siri ambayo hatujaijua.

Hata hivyo ninasikitishwa sana na mambo haya. Haiwezekani tusitumie vipaji badala yake kuwe na mtu mmoja anayefanya mazingaombwe kuwafanya wengine wafanye vizuri na wasio upande wake wawe wabovu.

Hivi vitu vitasababisha watu wengi tuchukie mpira wa nchi hii maana wengine hatuwezi kushabikia ushindani wa majini na binadamu.



Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Naungana na wewe..
Mkude saivi anawaka halafu Abdalah Hamis haonekani anachofanya..Kuna kitu behind the scenes
 
Yani nimekuelewa mnoo...kuna jambo ipo siku litasanuka...
Otherwise uongozi ufanyie marekebisho ya kiufundi yanayoonekana kwa macho...
 
Back
Top Bottom