Kuna tija gani kwa uharaka Uwanja wa Ndege wa Msalato?

Kuna tija gani kwa uharaka Uwanja wa Ndege wa Msalato?

Paf

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
1,703
Reaction score
3,307
Je, ni kweli wawakilishi wetu wapo kimaslahi ya nchi? KIA ipo, JKIA ipo, SGR hiyo inakuja.

Umataifa wa uwanja wa Msalato kujengwa kwa haraka huku watu wanakosa huduma za maji. Faida yake ni mini? Sifa.

Leteni kwanza faida za mbuga ya Chato.

Leteni faida za Tanzanite ya baharini.

Wabunge, hakuna vipaumbele?

Watoto hawana madawati, miaka 60 mnaongelea maji na upembuzi wakati mito imejaa vijijini huko.

MNATUCHOSHA SANA
 
Je, nikweli wawakilishi wetu wapo kimaslahi ya nchi.
KIA IPO,
JK DAR IPO,
Mji mkuu Dodoma, wangeni wa kinataifa watatua pale. Uliona wewe mwenyewe. Wakati wa mazishi ya kitaifa. Tulipata tabu kwa Marais waliudhuria. Uwanja aukutosha kuwapokea. Na Mabalozi wote wanatakiwa kukaa Dodoma
 
Umesahau kuwa uwanja huo upo makao makuu ya nchi? kwa hiyo wewe unataka Biden akija hapa atue kwanza Dar harafu apande treni? Njia zote 3 kuu za usafiri lazima zipatikane makao makuu ya nchi over. Watu wa Dar zipeni nafasi na sehemu zingine za nchi zipate maendeleo! miradi kibao Dar zaidi ya trillion moja inaendelea hapa watu wala hawalalamiki kosa msikie mradi nje ya Dar ndio tunakumbuka hakuna madawati,hakuna zahanati hakuna vyoo ili mradi tu hatupendi wengine wapate,khaa watu wa Dar acheni roho mbaya.
 
kwa kuwa makao makuu yameshakuwa dodoma basi uwanja wa kimataifa haukwepeki, japo ni gharama isiyo na msingi. Ingebidi kuliangalia hili wakati wa uamuzi wa kupeleka makao kule. Viongozi wa nyuma waliosita kuhamia huko pengine walioliona. Sio uwanja tu, kuna vingine vingi tu
 
Mbona ulivyojenwa uwa wa kimataifa wa Chato hamkuwahi kuongea
 
Ni upuuzi tu umeona Jiwe alijidai kukimbilia Dodoma matokeo yake alikua anashinda Dar na huyu wa sasa kila siku Dar hata leo naskia amerudi Dar ,hakukuwa na ulazima wowote wa watu kwenda Dodoma ulikuwa ni wazimu wa mwendazake tu, hivyohivyo na mamiradi yake yote yalikua upigaji tu
 
Dodoma kwenyewe hakuna hata maji baada ya miaka 60 ..pamoja na kuwepo DUWASA, WaterAID , nk nk....waazurura tu na magari yao
 
Dodoma kwenyewe hakuna hata maji baada ya miaka 60 ..pamoja na kuwepo DUWASA, WaterAID , nk nk....waazurura tu na magari yao
Na Dar awana maji pia. Maji mpaka atoke pwani. Hivyohivyo na Dodoma maji yatatoka kokote. Kwanza aujui Dodoma nadhani. Maji yapo
 
Back
Top Bottom