Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna jambo limenistua kidogo baada ya kusikia taarifa za bodi ya ligi kuhairisha mchezo kati ya Yanga na Simba kwa lengo la kwenda kufanyia uchunguzi madai ya Simba kuzuiliwa kuutumia uwanja wa Benjamini Mkapa kwa mazoezi siku moja kabla ya mechi. Tamko la Bodi ya ligi limetolewa masaa machache kabla ya mechi kuchezwa huku maandalizi yote muhimu yakiwa tayari yameshafanyika.
Hili ni tukio la pili ndani ya miaka mitatu, baada ya tukio la kwanza lilitokana na Yanga kugomea kuingiza timu uwanjani muda tofauti na uliotangazwa awali na TFF. Kipindi kile TFF ilifanya mabadiliko ya ghafla ambayo yalilalamiwa na Yanga kuwa yako kinyume na kanuni. Katika tukio lile, hakuna aliyewajibishwa na wala mchezo haukuhairishwa bali mchezo ulikuja kutangazwa tarehe nyingine ya kuchezwa.
Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
Kitu kilichonishtua ni namna TFF (bodi ya ligi) inavyoweza kuendesha shughuli zake kwa msukumo wa kufuata upepo wa hizi timu mbili za Simba na Yanga.
Kuna tukio liliwahi kutokea kwenye ligi yetu, ndani ya miaka miwili iliyopita, ambayo timu fulani ndogo ikiongozwa na kocha wake kugomea kuingiza timu uwanjani (pitch) ili ikaguliwe na mpira kuanza baada ya kocha wa timu husika kugundua uwanja ule haukuwa na Gari la kubeba wagonjwa (ambulance), jambo ambalo ni takwa muhimu la kikanuni kabla ya mechi yoyote kuchezwa ili kuhakikisha usalama wa afya za wachezaji uwanjani. Vyombo vya TFF vilikaa baadaye, kubariki timu husika kupokwa points na kumfungia kocha husika.