Mimi binafsi nimekulewa mkuu!Naona watu wanarukaruka ngoja muhenga niwape somo
Bukta ni brand name kama Nike. Zamani sana kaptura za michezo zilikuwa brand hio ndio maana hilo jina linatumika kwa kaptura nyingi za michezo. Ni kama vituo vya mafuta kuitwa sheli aka shell kwasababu ndio ilikuwa kampuni maarufu ya kuuza mafuta.
Pensi ni Pants Kiingereza. Pants inaweza kuwa short pants, 3/4 pants au long. Ni kama suruali.
Kaptura ni jina la jumla la suruali kipande. Kiingereza ni shorts.
Hahaha,, nmecheka sana aisee!Bukta ni nguo ya michezo fupi inayoishia magotini na kaptula ni nguo ya kuvaa fupi. Pensi ni aka ya kaptula