Kuna tofauti gani kati ya kuagiza gari nje ya nchi au kununua magari yanayouzwa 'yard' hapa nchini kwetu?

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Habari za kushinda wakuu?

Naomba kufahamishwa/kujulishwa tofauti iliyopo kati ya magari ya kuagiza nje ya nchi kwa mfano Japan, korea nk na yale yanayouzwa hapa nchini, unakuta mtu amefungua yard yake anauza magari ambayo ni used kama yale ambayo unaweza kuagiza kupitia makampuni mbalimbali yanayohusika na uagizaji wa magari,

Kwa mtazamo wangu gari inayopatikana hapa nchini unaikagua mwenyewe ukiridhika unalipia inakuwa yako, tofauti na yale ya kuagiza ambayo unaikagua kupitia picha au 'recorded video'

Mwenye uelewa anijuze kwa sababu naona kabisa kwa uweza wa Mungu naelekea kuwa mmoja kati ya wanaomiliki magari.

Natanguliza shukrani za dhati :4Shrug:
 
Inategemea na bajeti yako na aina ya gari unayotaka.
 
Chukua kama ipo Yard mkuu, kuagiza mara nyingi ni kama unataka mpya kabisa na haipo Yard na mara nyingi hata wanaogiza tunapitia kwa Dealers kwasababu ya uzoefu na kuepuka usumbufu.
Enzi hizo mwalimu wangu wa BAM aliniambia kuna utofauti wa Gari na Usafiri sijajua alichomaanisha kinaingia kwenye swali lako Ila Hongera sanaaa
 
Asante kwa shauri mkuu
 
Kuagiza unaweza kupata unafuu wa bei kuanzia 1,2,3m unaweza kuokoa.
Kununua yard unaokoa muda wa kusubiri gari,sasa hivi unaweza kusubiri miezi mitatu. Pia yard gari unaliona so hakuna surprises kama za kuagiza.
 
Utofauti upo...
Kama unataka kununua gari kwenye yard za bongo itakubidi uende kwa wauzaji waaminifu, wengi wao huwa wanabadilisha betri,spare tyres, fuse,taa,jeki na vitu vingine.
Pia wengine huwa wanashusha milage.

Wapo waaminifu ukienda kwao unapata gari kama ilivyo hasa pale mitaa ya namanga msasani.

Ukiagiza gari wewe mwenyewe Toka Japan utaipata kama ilivyo na bei pia itapungua kidogo ila usumbufu wa kuagiza gari ni kuisubiri Kwa kipindi cha mwezi mmoja Hadi miwili, alafu pia kuna Raha Fulani hivi unaipata ukiingia pale bandarini huku inakamilisha ishu ndogondogo za bandari ili uondoke na chuma yako
 
Enzi hizo mwalimu wangu wa BAM aliniambia kuna utofauti wa Gari na Usafiri sijajua alichomaanisha kinaingia kwenye swali lako Ila Hongera sanaaa
People are programmed to be consumers not producers. We take pride on using, spending, liability assets expenses none is proud of investing somewhere.
Lipwa salary ukaenjoi you're filling the hole that can't be filled since dawn and until dusk you won't fill it.

None is proud by leaving inheritance to his grandchildren
 
Kuagiza unaweza kupata unafuu wa bei kuanzia 1,2,3m unaweza kuokoa.
Kununua yard unaokoa muda wa kusubiri gari,sasa hivi unaweza kusubiri miezi mitatu. Pia yard gari unaliona so hakuna surprises kama za kuagiza.
Aisee sijui tatizo ni nini maana Mimi mwenyewe gari yangu ndiyo IPO njiani inakuja, ni zaidi ya miezi miwili imechelewa kwenye booking ya meli na hata wale dealer waliniambia kuwa shida ni usafirishaji tu
 
Utofauti upo...
Kama unataka kununua gari kwenye yard za bongo itakubidi uende kwa wauzaji waaminifu, wengi wao huwa wanabadilisha betri,spare tyres, fuse,taa,jeki na vitu vingine.
Pia wengine huwa wanashusha milage.

Wapo waaminifu ukienda kwao unapata gari kama ilivyo hasa pale mitaa ya namanga msasani.

Ukiagiza gari wewe mwenyewe Toka Japan utaipata kama ilivyo na bei pia itapungua kidogo ila usumbufu wa kuagiza gari ni kuisubiri Kwa kipindi cha mwezi mmoja Hadi miwili, alafu pia kuna Raha Fulani hivi unaipata ukiingia pale bandarini huku inakamilisha ishu ndogondogo za bandari ili uondoke na chuma yako
Nimekuelewa mkuu
 
Aisee sijui tatizo ni nini maana Mimi mwenyewe gari yangu ndiyo IPO njiani inakuja, ni zaidi ya miezi miwili imechelewa kwenye booking ya meli na hata wale dealer waliniambia kuwa shida ni usafirishaji tu
Kuna seasons za kuagiza magari, peak season huwwa kuna ucheleweshaji sana wa usafiri, ila kuna kipindi unakutana na zari la mentali, siku 40 tu chuma ipo kurasini hapo,
Gari ya kuagiza ina mzuka wake asee
 
Kuagiza unaweza kupata unafuu wa bei kuanzia 1,2,3m unaweza kuokoa.
Kununua yard unaokoa muda wa kusubiri gari,sasa hivi unaweza kusubiri miezi mitatu. Pia yard gari unaliona so hakuna surprises kama za kuagiza.
Nawajua watu wananunua yard tu maana kusubiri na zile paperwork process pamoja na simu nyingi anaona bora anunue chap yard,pia anasema yard hua bei inaweza ikaongezeka kidogo ila gari la uhakika sababu wale wa yard hawanunui famba,anasema wenye yard wengi(Pakistanis) hawategemei faida ya gari ila mishe nyengine so ni waaminifu.
 
Kuna seasons za kuagiza magari, peak season huwwa kuna ucheleweshaji sana wa usafiri, ila kuna kipindi unakutana na zari la mentali, siku 40 tu chuma ipo kurasini hapo,
Gati ya kuagiza ina mzuka wake asee
Ni kweli kabisaa aiseeee nakumbuka mwaka 2020 kipindi naagiza gari ilikuwa October gari haikuchelewa
 
Back
Top Bottom