infinix
JF-Expert Member
- Sep 6, 2018
- 2,096
- 2,150
Ndugu wanajukwaa la siasa,habari za jioni.
Naomba mnijuze kuhusu tofauti ya maamuzi ya kisiasa na kisheria. Mfano,wiki iliyopita,mh m bunge wa Kigoma,Zito R. Kabwe,aliita waandishi wa habari na kueleza msimamo wa chama chake kuhusu siasa,utendaji wa jeshi la polisi,hasa akizungumzia mauaji yaliyofanyika katka kijiji flani huko Kigoma hasa watu wa kabila la Wanyantuzu,alitaja idadi na pia wengine kwa mujibu wa maelezo yake waliuliwa wakiwa ndani ya hospitali.
Tunasikia polisi walimkamata,wakamhoji,na mwishowe wamempeleka mahakamani.
Kwa mawazo yangu ni kwamba,Zito ni mwanasiasa,hoja zake zimejikita kwenye siasa. Walichopaswa kufanya polisi ni kumjibu,ikiwa hayo matukio yalitokea au hayakutokea.
Hili tukio la kumkamata na kumpeleka mahakamani mimi binafsi sijaelewa msingi wake,au sababu yake ni nini..
Karibuni ndugu zangu kwa mjadala,natumaini tutatumia lugha nzuri ili kufahamishana kuhusu jambo hili.
Karibuni.