Marehemu
Tofauti ni nafasi aliyokuwa nayo huyo mtu kabla ya kifo chake. Katika hali ya kawaida kunawatu ambao tunawaita waheshimiwa. Yaani kila unapotaka kumtaja lazima uanze na Mh. Fulani, na pia wapo ambao hulazimiki kuanza na neno Mheshimiwa .... pindi unapotaka kumuita kwa jina, Hivyo basi tofauti hizi ndizo ambazo hupelekea kuwepo kwa matumizi haya ya Marehemu na Hayati katika nyakati tofautitofauti. Mtu ambaye katika uhai wake halitumiki neno Mheshimiwa basi akifa huitwa Marehemu,
Hayati
Kadhalika mtu ambaye hutumika neno Mheshimiwa ili kumuita, pindi akifa tunalazimika kutumia neno Hayati ili kuonesha kwamba bado tunaheshimu nafasi aliyokuwa nayo wakati wa uhai wake.
Tofauti katika matumizi
Kuna wakati inalazimika kuwepo kwa tofauti katika matumizi ya maneno haya. Mfano; unapotaka kumzungumzia mtu aliyekwisha kufa nje ya cheo au nafasi aliyokuwa nayo katika jamii basi litatumika neno Marehemu na si Hayati. Kwa mfano: tukimzungumzia Edward Moringe Sokoine nje ya nafasi aliyokuwa nayo wakati wa uhai wake tutasema Marehemu Moringe Sokoine ali........... Lakini tutakapokuwa tunamzungumzia katika nafasi ya uheshimiwa wake tutasema Hayati Moringe Sokoine ali.........
Ikumbuke haya yote si sheria ila ni utaratibu tu katika lugha, ambao umechukua nafasi kutokana na mazoea yaliyopo katika matumizisahihi ndani ya jamii zetu.