Kuna tofauti gani kusoma law tanzania na nje ya tanzania?

Just Distinctions

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2016
Posts
3,230
Reaction score
6,742
Habari zenu wakuu, natumai nyote ni wazima. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi nina lengo la kusoma sheria ila katika mchakato wangu ninatafuta chuo nje ya nchi na malengo yakiwa ni ujerumani, canada au china. Lakini swali langu ni kuna utofauti gani wa kusoma sheria nje ya nchi na hapa?, je kuna vitu huwa vinatofautiana maana dira ni kuwa baada ya kuhitimu ikiwa ntafanikiwa kupata chuo, nirudi hapa nyumbani na kufanya kazi, vipi kuhusu school of law baada ya kuhitimu? Maswali ni mengi ila natumai mtanisaidia kwa haya na mengine ntauliza kadri nitakavyoona inafaa, natanguliza shukrani.
 
Kwa commonwealth countries principles ni karibia zile zile, ila utofauti ni sheria za ndani tu, hata kwa nchi nyingine ambazo hazikutawaliwa na malkia kanuni za kisheria ni karibia zile zile tu, hakuna utofauti mkubwa.

Kwa mfano sisi hapa Tanzania,tumekopi kwa asilimia kubwa sheria za India, ambazo ndiko Uingereza walitaka kufanyia majaribio ya matumizi ya sheria zilizoandikwa.
 
kwa hiyo maana kusoma kwangu nje hakutonisababisha kutofanya kazi kwa ufasaha hapa nchini, bali katika kipengele cha ndani?, na je kwa ushauri wako we unaona ni vema niendelee na mpango wa nje au itakuwa ni bora zaidi nikisoma hapa tz?, asante.
 
Haitaathiri HATA KIDOGO utendaji wako utakapoamua kuja kufanya kazi hapa nchini but nakushauri usome Canada na kama utalazimika kusoma kwingine fanya utafiti ufanye LL.B kwa chuo ambacho TCU na Council of Legal Education vinakitambua ili uweze kusoma Law School hapa nyumbani. Wengi tu wamesoma Bachelor nje na kumalizia hapa taaluma yao.
 
Nje unapata Exposure ambayo hapa hutoipata, halafu chengine nje watu hawasomi msuli pepa kuelewa lazima paper sio za kukomoana, unapata muda mwingi wa kukaa na lecturer wako akauelekeza vitu ambavyo huvielewi n.k Nakushauri tafuta Scholarship kasome nje mkuu
 
kwa hiyo maana kusoma kwangu nje hakutonisababisha kutofanya kazi kwa ufasaha hapa nchini, bali katika kipengele cha ndani?, na je kwa ushauri wako we unaona ni vema niendelee na mpango wa nje au itakuwa ni bora zaidi nikisoma hapa tz?, asante.
Hakuna madhara yeyote, nenda tu mkuu..
 
Back
Top Bottom