Hivi Ndugu huu mjadala umeudakia njiani ama umeanza nao mwanzo ukajaribu kuelewa vizuri? Na je unaweza kutofautisha kati ya Shabiki na mtu kama wewe. Je kuanza Hip Hop mwaka 1988 (Which i doubt maana sijui kama ilikuwa hapa Bongo ama somewhere else maana miaka hiyo....3 years after utawala wa Nyerere mengi yalikuwepo). You should know this I am Hip Hop.
Katika game ya Muziki ya Tanzania nimekuwa nayo toka inaanza. Nimekuwa na hawa Artists wa Bongo toka wakiwa katika Mihangaiko ya kutoka na kutafuta maana na uhasilia wa Muziki wao ambayo sidhani kama wameipata. Umeongelea Sumbawanga, sisi tumefanya Show Sumbawanga miaka ile unafika na kukutana na Nyimbo za Mr II (Sugu) pekee maana ni album yake tu ndo FM waliweza ifikisha kule. Mimi ni shuhuda wa Muziki wa Bongo wa Kizazi Kipya toka mwanzo mpaka muda huu. Nilichokuwa najaribu kukufahamisha ni kwamba huwezi Mcrown Sugu ati Godfather wa Bongo Flava!!! Utakuwa unamtusi kikuu. Katika kuhakikisha Hip Hop ya Bongo inasimama ndo maana SUGU mwaka 2005 alikuja na HIP HOP SUMMIT YA TANZANIA! Na pia nilikuwa Key Player katika hilo. Unataka nikuambie ni nini yalikuwa madhumuni na Madhumuni ya hiyo SUMMIT?
Hakuna mtu aliyemuona FA ama Matonya ni wajinga ama Kikosi, Adili na Fid Q wamepotea njia katika aina ya Muziki wanayofanya. Hili ni jambo la kufahamu ni nini haswa ambacho unataka ku-achieve katika yote ufanyayo.
Unaongelea vijana wa mjini na mikoani unajua nini juu ya hilo? Unafahamu aina ya Muziki inayofanywa na undergrounds wa Mikoani kwa kiasi kikubwa ama? Unafahamu haswa muziki wa Bongo unaendaje wewe? Na unafahamu hivi kuna aina ngapi za muziki zinafanya Bongo Flava ama?
Mwisho unasema vurugu yote ilikuwa ni Mwangwi wa Wanamuziki wa Marekani (Weusi), huoni kwamba ilikuwa si mwangwi (Echo) maana eventually mwangi hupotea, kinachofanyika kila siku ni kuchukua Muziki wa Kigeni na Kujaribu ufitisha katika Jumuia ya Bongo na kufanya tuwe na identity yetu.
Fikiri kwa umakini kabla ya kujibu!
SOME GOT WAYS AND MEANS, WE GOT HOPES AND DREAMS!