Mie naona sawa tu. Anaweza kuwa mfalme ila madaraka yake yawe wamepunguzwa. Kazi zote za kiserikali ziwe chini ya Waziri Mkuu kama ilivyo Spain, UK, Sweden, nk.
Ila wasiwasi wangu mie ni mmoja:
Watu kama Ruge, Makamba childrens, Kusaga etc yaani kwa ufupi Watoto wa MUJINI, wanaweza wakaja na mawazo yao mapya ya kumuingiza mfalme wetu mjini. Kibaya zaidi kinachoweza kutokea ni KUMNUNULIA vazi zito sana mfalme wetu, vazi ambalo hakuna mtu yeyote duniani ameshawahi kulivaa, vazi la bei mbaya sana. Vazi hilo, materials zake ni aghali sana, ila ni zuri mno, itabidi tulinunue hata kama ikibidi tule nyasi. Ili kuonyesha tofauti na mavazi mengine duniani, hili vazi litakuwa halionekani yaani Invisible.
Itakuwa furaha kumuona January Makamba na Ruge wakimvisha Mfalme wetu vazi lisiloonekana, na yeye akiendelea ku-smile. Huo mie ndiyo woga wangu maana watoto wa siku hizi, watamwaga radhi palepale.