Uchawi ni Imani yako Mkuu, ukiamini inakuwa, Imani ina nguvu, mimi nimeshawaambia watu mara zaidi ya 10 kuwa kama uchawi upo wauthibitishe hata kwangu, waniroge wawezavyo wakitaka mate yangu, kucha, kipande cha nguo au nywele waje kuchukua.
Uchawi ungekuwepo wakoloni wasingeweza kutesa babu zetu kiasi cha kuwafanya mababu wanne wa kiafrika wambebe mtawala mmoja mweupe kutoka kigoma mpaka Kilimanjaro kulima na kupalilia mkonge.
Uchawi ungekuwepo wachezaji wa kinigeria wangekuwa wanashinda kombe la dunia kila wanaposhiriki, Simba ingefika rank ya Barcelona na zaidi.
Lakini USHINDI na hata UTAJIRI unategemea zaidi JUHUDI, BIDII na MAANDALIZI.
Sanasana Uchawi ni story za kutungwa zinazosambazwa na watu tu kutoka sehemu moja mpaka nyingine na kuaminiwa.
Soma kitabu kinaitwa
'' Faith can change your World'' cha Lister Sumrall, utaelewa sana hii kitu.