- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumetokea uvumi unaosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na uwepo wa ugonjwa hatari nchini CONGO DRC.
Ugonjwa huo unasemekana kuenea na kuambukizwa zaidi kwa njia ya ngono.
Pia inasemwa muathirika huugua kwa kipindi Cha muda mfupi sana (kati ya siku 4 Hadi wiki 2) Hadi kupoteza maisha.
Naomba wanajukwaa na JamiiForums kwa ujumla tusaidiane kuhakiki habari hii ambayo imekuwa ikisambaa kwa kuambatana na sauti inayoelezea ugonjwa huo pamoja na picha za waathirika na watu wakifanya mazishi (ya anayesemekana kafariki kwa ugonjwa huo) huku wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga mawili mzma na kuacha sehemu ya uso tu.
TAHADHARI: Baadhi ya picha sio nzuri kutazama hadharani. Naomba radhi kwa hilo, nazi-attach kama nilivyozipokea ili wote tupate picha halisi.

- Tunachokijua
- Kumekuwepo na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa zimeambatana na ujumbe wa tahadhari ya uwepo wa ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya ngono uliotokea Goma, Uvila, Bukavu Nchini Kongo, zikionesha ugonjwa huo ukishambulia kwa kusababisha mapele yanayosababisha vidonda sehemu za mwili ikiwemo sehemu za siri na kinywani.
Picha hizo zimeonesha watu wakiwa wamevaa mavazi maalum huku wakieleza kuwa hao ni watu wanaozika miili iliyopatwa na mauti kutokana na ugonjwa huo na wakidai mtu aliyepata ungonjwa huo huishi muda mfupi kati ya siku 4 hadi wiki 2 na kisha hupoteza maisha.
Je, ukweli ni upi kuhusu taarifa za uwepo wa ugonjwa kama huu nchini Kongo?
Picha hii inadaiwa kuwa ni ya mgonjwa wa ugonjwa huo wa ngono nchini Kongo
JamiiCheck imefatilia taarifa za uwepo wa ugonjwa ambao unadaiwa kutokea nchini Kongo na kubaini kuwa taarifa hizo si za kweli, Picha zinazotumika kuelezea ugonjwa huo ni picha za watu waliopata ugonjwa ujulikanao kama monkeypox ambao ugonjwa huo umekuwepo Kongo kwa kipindi kirefu, Januari 1 2023 Kongo iliripoti zaidi ya wagonjwa 20000 na vifo 1000 kutokana na ugonjwa huo.
Virusi wa ugonjwa huu ni jamii moja na virusi waliokuwa wanasababisha ugonjwa wa Ndui(smallpox) ugonjwa huu hutokea mara nyingi nchi za Afrika ya Kati na Afrika Magharibi, mwaka 2022 matukio ya ugonjwa huu yaliripotiwa nje ya Afrika kwa mara ya kwanza huko Uingereza na Marekani na unaambukizwa kwa kugusana, ikiwemo na ngono na nyingine ni za magonjwa mengine, picha zinazoonesha watu waliovalia mavazi maalum zilipigwa kipindi cha mlipuko wa UVIKO.
Baadhi ya wataalamu wa afya wamejitokeza na kukanusha kuwa picha hizo si za ugonjwa mpya bali ni monkeypox na magonjwa mengine.
Pia, JamiiCheck imefuatilia vyombo vya habari mbalimbali nchini Kongo ikiwemo na Wizara ya Afya ya Kongo ambapo hakuna taarifa yoyote ya uwepo wa ugonjwa huo kama ambavyo unadaiwa kuwa umezuka nchini humo na hivyo tunathibitisha kuwa taarifa hizo ni za kuzusha.