Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,006
- 13,281
Kwaio soka lisiendelee kisa machotara na akilimali hawatojulikani watakula wapi...!?Mzee akilimali akale wapi?
Wale machotara wataheshimiwa vipi?
hili swala sio la kuamka kesho na kutoa maamuzi...1.Yani ufungue kampuni then ndio uje uwaelimishe wanachama ?
2.What is so special with kampuni ? Tupe mifano
3.Timu zinapangwa na viongozi au wanachama (Kaburu,Hans Pope,) ? Tupe mifano ya hao wanachama unaosema
Real Madrid,Bayern Munich,Barcelona ni timu zinaendeshwa na wanachama na zina mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja
hili swala sio la kuamka kesho na kutoa maamuzi...
ni swala la mikakati... lazima elimu itoke ili watu wawe na uelewa...
Hata hao madrid unaosema serikali iliingilia kati.. na kupitisha sheria ya kila timu ziwe private owned company...
Hata hio madrid ilibidi itoe vielezo vya kutosha kama itaweza kuendeleza mfumo wa wanachama.
Hao wanachama wapo pale kwa manufaa ya Club kuanzia uongoI mpaka wachezaji..
Je hizi timu zetu wanachama wanaweza hivyo... wanaweza kua hapo bila kuingilia uongozi wa timu.
asilimia kubwa ya timu za nje zina mfumo wa kikampuni na zinafanikiwa...
FC United of Manchester - Organisational Structure
Pitia link uangalia structure ya man u.Nina uhakika timu zetu zikibadilisha mfumo zitafanimiwa kwa 100%.
je huu mfumo uliopo sasa ambao unasababisha hakuna hata miradi ya maendeleo.. utaweza kufanikiwa…?
Ni miongo mingi sasa huu mfumo upo lakini kila siku unazidi kuua soka letu..
Uspecial wa kampuni unakuja kwenye kutimiza malengo na mipango ya kampuni na uraisi wa kutekeleza maagizo yanayotolewa na vyombo vinavyo oongoza soka...Idea ya kampuni inaondoa umiliki wa wananchi wenye hali ya chini /wazawa na kufuta utamaduni wa timu (umeona Liverpool,Man United ) hao wenye hisa priority yao ni pesa tu.Huwezi ukaanza kupropose kufungua kampuni kwa klabu kama Yanga/Simba ambazo wanachama hai hata laki moja hawafiki.Watu ambao wanashindwa kufanya hata audit ya mapato na matumizi wafungue kampuni
Again what is so special with kampuni ?
Jibu hilo swali kwanza
Uspecial wa kampuni unakuja kwenye kutimiza malengo na mipango ya kampuni na uraisi wa kutekeleza maagizo yanayotolewa na vyombo vinavyo oongoza soka...
hapa linakuja swala la kurasimisha mochezo na kua kazi kama kazi zingine....
Structure ya kampuni itatoa mgawanyo wa kazi kulingana na nafasi na uweledi wa mtu.
usimamizi mzuri wa projects za timu kuanzia shule za kuendeleza vijana kila timu.. mpaka timu Za watoto timu B na timu kubwa.
Usimamizi mzuri wa fedha na miradi mingine ya timu.
upangaji wa mishahara kulingana na nafasi.
hili litasaidia wafanyakazi waweze kujiunga na mifuko ya mafao.
Uendeshwaji wa timu utakua wa kisomi.
wadhamini wengi watajitokeza na si kutegemea mzamini mkubwa wa Ligi.
Hapa hizi timu pamoja na wachezaji zitakua brand tofauti na sasa hivi wavhezaji tuna wachukulia watu wa kawaida tu wenye uwezo wa kucheza mpira.
lazima club zisimamie ziwatunze na kuwalinda wachezaji kama bidhaa zao zinazowapatia faida kama kampuni.
Hizo ni baadhi ya uspecial wa kampuni...
Niambie ni kipi kimefanimiwa au kinaweza kufanikiwa kati ya hivyo kupitia mfumo wa sasa hivi na aina ya watu tulionao ndani ya vilabu na soka kwa ujumla.....!?
Hahaha... jamaa unaongea nini... hakuna lisilo shindikana....Unaongea mambo ya dunia ya kwanza wakati tuko dunia ya tatu.Unapaswa kuanza kutumia rasilimali ulizonazo kwanza
Usimamizi wa hauanzii kwenye kampuni,kama haya mambo madogo wanashindwa unafikiri kampuni ndio itaondoa hayo matatizo.
Kampuni ngapi zimefunguliwa na zimekufa