Ah ah aha ha haya maswali mengine bana!, labda ni kutokana na kila kitu kilivyo testi yake inakifanya kiendane na chumvi au sukari. Ila ktk chakula chumvi ndio pekee inayoleta ladha katika vyakula vingi zaidi, sukari pia ina nafasi yake mfano: wapo wanaoweka sukari katika makande, tambi, au futari, lakini sio wote wanaopenda, wengine hutia chumvi ktk makande, tambi au futari.
Chumvi ina ugwadu fulani hivi ambao huleta utamu ktk baadhi ya matunda hasa embe mbichi, tango, parachichi sio lazima labda upende tu mwenyewe. Chumvi inaleta raha kubwa sana ktk vyakula vya aina yake, na kubwa zaidi ni kujaribu kukila kitu na chumvi ndo utajua kama kinaendana au vipi, mfano:- Mahindi ya kuchoma hayakua yakiliwa na chumvi, lakini siku hizi full chumvi, ndimu na pilipili, nani aligundua ni ubunifu tu wakusaka wateja.
Pia binafsi huwa naweka chumvi ktk chungwa tamu kabisa, na ninafeel good kulila. So inategemea na ladha ya tunda au chakula chenyewe na mlaji pia, wengine hawapendi kabisa chumvi anaweza kula embe chachu hivyo hivyo.