Kuna uhusiano gani kati ya Clouds FM na E-FM?

Kuna uhusiano gani kati ya Clouds FM na E-FM?

Nedago

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2018
Posts
908
Reaction score
1,350
Nimekua nikiona mara kwa mara hivi karibuni event nyingi za harmonize basi Cloud's TV na TV-E wanarusha live,tofauti na vituo vingine,

Na hata Show's nyingi bure za pale nyuma kidogo baada ya konde boy au aka Tembo au jeshi,kujitoa WCB wasafi,clouds na E-fm walikuwa very close na harmonize.

Na ukiachana na hilo la vituo vyote hivyo viwili kuonekana vimeungana kumsapoti konde,nimekuwa nikiona comment's humu na kusikia tetesi kwenye vijiwe vya kahawa na mitaani kuwa yule bwana majizzo,CEO Na MD wa E-fm anapewa kipaumbele cha kwenda kuchukua nafasi ya ruge pale cloudsfmtz

Je kama majizzo ni Mmiliki wa E-fm anawezaje kwenda kuwa mhimili wa kituo pinzani cha burudani?
Au majizzo pale E-fm ni kimvuli tu,kuna wamiliki wengine? Maana Mimi muda wote nimekuwa najua kuwa majizzo ana miliki E-fm na TV-E kwa asilimia 100,sasa napata ukakasi juu ya hizo tetesi na uhusiano wa cloudsfmtz na E-fm.

Au kusaga pia ana hisa pale E-fm?
Ndio maana hivi vituo vimekuwa close hivyo?

Au inawezekana vimeamua kumsapoti kondeboy huku kila mmoja akiwa na target ya kumtumia kwenye msimu ujao wa matamasha ya kiburudani Yaani fiesta na mziki mnene?na Je hilo haliwezi Baadae kumuweka kondeboy njiapanda hasa msimu wa Show's kuanza.
 
Hizo ni hisia Zako tu Wala hakuna Ukaribu Wowote, Kuhusu Swala la kurusha Live Inategemeana na Makubaliano Yao na Msanii
 
Kurusha matangazo ni mpunga wako tu we unadhani event kama Ya jana ya Harmonize ime rushwa bure?Majizo kuchukua nafasi Ya Ruge clouds sio kweli story zenu za vijiwen za kisu biria msosi hizo.
 
Nikiri nilishawahi kumsikia KUSAGA akisema radio nyingi zilizoanzishwa na vijana kuna mkono wake kwa namna moja au nyingine ila napata ukakasi na kutojua hadi leo alikuwa ana maana gani.

Ila inawezekana vipi aka monopolize station za radio zote mpya.
 
Hapo ndio haijulikani ila nahisi yupo pale pia?
 
CRDB wamelipia wanajua ndio TV zenye watazamaji wengi kwa sasa
 
Yule c don
Nikiri nilishawahi kumsikia KUSAGA akisema radio nyingi zilizoanzishwa na vijana kuna mkono wake kwa namna moja au nyingine ila napata ukakasi na kutojua hadi leo alikuwa ana maana gani.

Ila inawezekana vipi aka monopolize station za radio zote mpya.

121.
 
That's nonsense, yaani aondoke nyumbani ambako ni kuzuri tayari aende kuomba makazi kwa jirani? Hizo kweli story za kahawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom