Kwa ufupi sana ni hivi. Kwanza lazima uelewe HIVAIDS ni nini. HIV/AIDS inalenga kushambulia na kufumaza kinga ya mwili. So mtu akishakuwa na HIV/ AIDS kinga ya mwili inashuka. Sasa kumbuka kuna vimelea vya magonjwa mengine yanayosababishwa na Bacteria, Fangasi na Virusi huwa mtu anakuwa navyo. Lakinintu kwa kuwa kinga ya mwili kwa mtu asiye na HIV/AIDS inakuwa juu, basi inapambana navyo. Ila pale sasa kinga inaposhuka Vimelea hivi huchukua hatamu sasa na kuanza kushambulia mwili. Moja ya vimelea hivyo ni hivi vinavyosababisha TB yaani Mycobacterium Tuberculosis. Kimsingi kila mtu kutoakana na mazingira ana hivi vimelea. Na ndio maana hata watoto wadogo wanapozalowa huwa tunawapa chanjo inaitwa BCG ili kuwakinga wasipate mashambilizi ya vimelea hivi sababu kinga zao bado zinakuwa chini. Hii ndio sababu kubwa mkuu. Nadhani nimejaribu kueleza kwa lugha rahisi sana.