Kuna uhusiano gani kati ya hofu/wasiwasi na tumbo la kuharisha?

The Businessman

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
7,397
Reaction score
9,255
Amani iwe kwenu,

Naomba mnujuze kuna uhusiano gani kati ya wasiwasi au hofu na kuanza kuuma kwa tumbo? Kwanini nimeuliza hivi, Ni mara nyingi hii hali hunikuta .

Pia hata ndugu zangu huwakuta pindi wanapopatwa na hofu kwa mfano, kuna mama hapa kapata habari kuwa binti yake wa kidato cha pili amepata mimba ghafla tu yule mama alianza kulalamika tumbo linamuuma.

Nauliza
 
utumbo huwa unaruka unapo pata wasi wasi au taarifa mbaya sasa kwa kuwa utumbo haupo sawa basi lazima uumwe kwa mda
 
Kuna rafiki yangu kipindi cha UE somo likiwa gumu alikua anapaniki mpaka tumbo kumchafuka Mpaka tulikua tunacheka.
Nadhani ni uoga na paniki. Ngoja wajuzi waje kutujuza
 
Hata kwangu ni kawaida sana sijui kuna mahusiano gani... kwenye pochi yangu hukosi dawa za maumivu ya tumbo na kuzuia kuharisha.
 
Kitaalamu tunaita 'psychogenic diarrhea' inawapata watu wengi wakiwa na stress, woga au anxiety. Uhusiano kuelezea lazma itabd niingie kiundani kwny the physiology behind...ila sio ugonjwa na hupotea mara baada ya kutoka au kupita kipindi husika
 
Hata Mimi jamani,, imenitokea Mara nyingi sana! Lakini pia kuna uhusiano gani na mtu anapofariki rafiki ndugu au jirani kupata Shida, mfano Mimi kama kuna mtu namfahamu hata kama sina uhusiano nae wa damu. Na hata kama sifahamu km ni mgonjwa siku 2/3 kabla ya kufariki mtu huyo Naumwa tumbo na kukata pia huwa siwezi kushiba!hivi ni ugonjwa au kawaida
 
Hii hali hunipata Mara nyingi sana hadi huwa naogopa kupokea simu za watu ninazohisi hazina heri kwasababu ya kuogopa kuumwa tumbo na kuharisha.
 
Ata mimi wakati wa kupata matokeo au nikpata msh2ko naharisha sana ata hapa nimesh2ka
 
Nyinyi nyote valve seal zenu zimeloose sababu ya kula na kupitisha vitu vigumu michonyoni kwenu huko

Over
 
Hata bavicha hiyo hali wanayo sasa hivi kisa dr haonekani. Hiyo hali huwa inaambatana na kuropoka/ kutukana hovyo pamoja na kuishiwa nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…