Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu utakuwa unajua uhusiano kati ya gari na dereva? ukijibu hilo utapata na jibu uliloliomba. bila dereva gari yaweza kwenda?hsbari wanajamvi tafadhalini naomba ufafanuzi mwendesha mashtaka pp ana uhusiano gani na kesi naulixa hivi nikiwa na maana hii kesi inaweza kuahirishwa kwa sababu pp hayupo?
mkuu utakuwa unajua uhusiano kati ya gari na dereva? ukijibu hilo utapata na jibu uliloliomba. bila dereva gari yaweza kwenda?
lakini kutokana na specification yako, pp ni republic, ni mwanadamu ambaye leo anaweza awepo au asiwepo, na jalada la kesi yeye ndio alilisoma vizuri kwaajili ya kuendelea, akija pp mpya itakuwa sio fair huyo mpya kuendelea na jalada ambalo hajalisoma. inaweza kuahirishwa either huyo pp mpya aliyekuja kuahirisha akalisome jalada ili tarehe ijayo mje muendelee au kama amesoma mtaendelea. hivyohivyo kwa wakili wa kujitegemea, kama umeingia katikati, itakuwa sio fair kama utaendelea bila kusoma proceedings, utalipua na utasababisha haki isitendeke, ndio maana huwa tunaomba proceedings ili tuzisome kesi iliendeleaje ili aendelee kwa uelewe. huwezi kuendesha jalada ambalo haulijui vizuri. kwahiyo kama pp mpya ameahirisha jalada ambalo hakuwa analiendesha yeye kwasababu pp aliyeliendesha jalada hilo hayupo. au nikujibu nini tena kingine?
wakili wa serikali au public prosecutor yeyote anao uwezo chini ya kifungu cha 91(1) au 98(a) CPA kuondoa shitaka. wanafanya hivyo kwasababu wanaact kama mawakala wa dpp mwenye uwezo wa kufanya hivyo au pengine waweza kufanya baada ya kuwasiliana naye. wakati kesi ikifunguliwa na ikaendelea ni kawaida kwa mwendesha mashitaka akiona kuna mshitakiwa hana ushaidi wa kutosha, anaweza kumuondoa na kubadilisha hati ya shitaka iwe na wale waliobaki tu. kwa hiyo hapo jibu ni NDIYO.okey asante kwa majibu yako maxuri hute itakuea vyema kama utanisaidia na hili je pp ana.uwezo wakumuondoa mtuhumiwa kwenye shitaka? na je kwa kawaida upelelezi unatakiwa ukamilike ndani yamuda gani baada ya kesi kufika mahskamani? na n hatua gani mtu aliyeingizwa kwenye mkumbo wa kesi isiyomuhusu anatakiwa kuzifuata ili apate haki yake ya msingi? n hayo tu muheshimiwa naomba msaada wako.
wakili wa serikali au public prosecutor yeyote anao uwezo chini ya kifungu cha 91(1) au 98(a) CPA kuondoa shitaka. wanafanya hivyo kwasababu wanaact kama mawakala wa dpp mwenye uwezo wa kufanya hivyo au pengine waweza kufanya baada ya kuwasiliana naye. wakati kesi ikifunguliwa na ikaendelea ni kawaida kwa mwendesha mashitaka akiona kuna mshitakiwa hana ushaidi wa kutosha, anaweza kumuondoa na kubadilisha hati ya shitaka iwe na wale waliobaki tu. kwa hiyo hapo jibu ni NDIYO.
upelelezi unatakiwa kwisha lini?...inategemeana na aina ya kosa. kuna makosa mengine ambayo upelelezi haujawa specified kwamba unatakiwa uishe lini. mfano, forgery na mengine kasome 225 (4) CPA, kuna makosa ambayo yameorodhesha kuwa hayana kikomo. vilevile kuna makosa mengine yapo subordinate courts kama preliminary inquiries kusubiria upelelezi uukikamilika washitakiwa wawe committed to the high court, that means mahakama za chini hazina mamlaka kuendesha wala hata kulifuta, hapo itabii uwe mpole usubirie tu hadi upelelezi uishe kama republic watakavyotaka. mfano, kesi za madawa ya kulevya, mauaji, economic crime cases n.k.
ila kuna makosa yale ambayo ya kawaida, hayajatajwa kwenye kifungu hicho hapo juu, upelelezi wake unatakiwa kuwa umeisha ndani ya siku 60, kama republic wataona bado haujakamilika basi kabla ya siku 60 hazijaisha wanatakiwa kufile certificate ya RCO kuomba kuongezewa siku 60 nyingine. siku 60 zikiisha na bado wanatakiwa kufile certificate ya State attorney kuongeza siku 60 nyingine, hizo za state attorney zikiisha wanatakiwa kuleta certificate ya dpp ambaye amepewa uwezo wa miezo 24 (miaka miwili). piga hesabu hapo uone namna republic wakiamua kukushughulikia watakachofanya. 60 zile za mwanzo kabla ya rco plus 60 za rco plus 60 za state attorney plus 24 months sawa na miezi 30. unao uwezo kukaa ndani kwa miezi 30 yaani miaka miwili na nusu unaweza kukaa ndani tu kama wakiamua.