Kuna uhusiano gani kati ya maziwa na vumbi?

Kuna uhusiano gani kati ya maziwa na vumbi?

nziriye

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
1,050
Reaction score
363
Habari zenu wakuu?

Mie nimekuwa nikiwaza uhusiano uliopo kati ya kunywa maziwa na kupunguza vumbi ulilovuta,utasikia ukifanya kazi ktk eneo lenye vumbi kunywa maziwa.

Please wadau i need to know what is the scientific/biological relationship btn drinking milk and cleaning of dust inhaled
 
Hiyo ya kuwapa wafanyakazi maziwa ni njia tu ya kukwepa kuwajibika kwa mwajiri. Scientifically, mwili wa binadamu ukiwa na afya njema unaongezeka uwezo wa kustahimili maradhi. Hivyo kunywa maziwa haina tofauti na kula nyama ama maharagwe. Lakini maziwa yanaenda kwa tumbo, sumu itaenda kwenye ini, vumbi ni mapafu. Hakuna uhusiano hapo zaidi ya kuepuka utapiamlo.

Ukiangalia 'risk analysis', na mikataba ya ridhaa duniani, inapaswa kukabiliana na hatari zilizopo kwanza kwa kuziondoa kabisa (elimination). Iwapo haiwezekani kufanya substitution kwa kutumia malighafi ama njia iliyo salama zaidi. La ikishindikana basi engineering itumike (kama ni vumbi litolewe na exhaust, kama ni sumu itengwe ama kutumika kwenye chamber maalumu).

Hatua hii ikishindikana basi inatakikana kutumia 'management controls', maana yake wafanyakazi waelimishwe madhara, jinsi ya kujiking, wapewe vifaa kinga na pia kuangaliwa afya mara kwa mara.

Kwa ujuzi zaidi google 'risk assessment' utapata material mengi ya kukuelimisha zaidi. Kiufupi kupewa maziwa uvutishwe sumu ama vumbi ni kutapeliwa. Muambie mwajiri aondoe vumbi, awape na kinga na maziwa juu yake.
 
Hiyo ya kuwapa wafanyakazi maziwa ni njia tu ya kukwepa kuwajibika kwa mwajiri.
Scientifically, mwili wa binadamu ukiwa na afya njema unaongezeka uwezo wa kustahimili maradhi. Hivyo kunywa maziwa haina tofauti na kula nyama ama maharagwe...
okey i wil google it.
 
Na ni njia ya wafanyakazi kutaka kunywa maziwa; ambapo si rahisi kuyapata manyumbani kwao
 
mbona mtu akinywa sumu anapewa maziwa? maziwa yanasaidia sana mwilini,yanasafisha
 
Maziwa hayana uhusiano wa moja kwa moja na vumbi, isipokuwa kupitia mate mazito ndani ya mfumo wa kinywa na koo (mucus). Mate haya (mucus) ndio yana uwezo wa kudaka vumbi, moshi, vimelea vya magonjwa, na hewa yoyote chafu inayopita kinywani na kuipeleka tumboni bila kudhuru viungo vilivyo njiani. Kadri mate haya anavyozidi kuwa mazito, ndivyo uwezo wake wa kudaka na kupeleka uchafu huo inavyoongezeka.

Sasa basi, tafiti mbali mbali zinaonesha kuwa unywaji wa maziwa unasababisha mucus kuwa nzito zaidi na hivyo kuongeza uwezo wa kudaka vumbi. LAKINI, "uzito wa mucus" na "uwepo wa mucus ya kutosha kubeba vumbi lote unalovuta" ni vitu viwili tofauti kwa maana kuwa unaweza kunywa maziwa wakati huna mucus ya kutosha.

Ndio maana njia za kuzuia uvutaji vumbi mahala pa kazi, kama alivyoainisha King'asti, ni muhimu sana kuzingatiwa. Vile vile, unywaji maziwa unasisitizwa wakati wote pasi kusubiri baada ya kuvuta vumbi kwa sababu zaidi ya kuwa na virutubisho vingi vya mwili lakini hata wavuta vumbi wanafaa kunywa maziwa long before uvutaji wenyewe.
 
Asanteni wakuu kwa mawazo yenu. Nashukuru Google kunileta kwenye Huu Uzi. Nami niufufue kwa faida ya wengine.
 
Ni njia mbili ambazo haziingiliani,huwezi kuondoa vumbi kwa kunywa maziwa.
 
Back
Top Bottom