Hiyo ya kuwapa wafanyakazi maziwa ni njia tu ya kukwepa kuwajibika kwa mwajiri. Scientifically, mwili wa binadamu ukiwa na afya njema unaongezeka uwezo wa kustahimili maradhi. Hivyo kunywa maziwa haina tofauti na kula nyama ama maharagwe. Lakini maziwa yanaenda kwa tumbo, sumu itaenda kwenye ini, vumbi ni mapafu. Hakuna uhusiano hapo zaidi ya kuepuka utapiamlo.
Ukiangalia 'risk analysis', na mikataba ya ridhaa duniani, inapaswa kukabiliana na hatari zilizopo kwanza kwa kuziondoa kabisa (elimination). Iwapo haiwezekani kufanya substitution kwa kutumia malighafi ama njia iliyo salama zaidi. La ikishindikana basi engineering itumike (kama ni vumbi litolewe na exhaust, kama ni sumu itengwe ama kutumika kwenye chamber maalumu).
Hatua hii ikishindikana basi inatakikana kutumia 'management controls', maana yake wafanyakazi waelimishwe madhara, jinsi ya kujiking, wapewe vifaa kinga na pia kuangaliwa afya mara kwa mara.
Kwa ujuzi zaidi google 'risk assessment' utapata material mengi ya kukuelimisha zaidi. Kiufupi kupewa maziwa uvutishwe sumu ama vumbi ni kutapeliwa. Muambie mwajiri aondoe vumbi, awape na kinga na maziwa juu yake.