Kuna uhusiano wowote wa ndevu kwa mwanamke na kuzaa ama kutozaa

mkuru

Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
22
Reaction score
8
Mwenye uelewa na hili tafadhali atujulishe itakua msaada kwangu na kwa wengne
 
Inaweza kuhusiana kwa kiasi fulani wanawake wenye ndevu wana muongezeko wa homoni za kiume testerone kwenye mwili na ndio maana wanapata characters za kiume kama hio kuota ndevu,sauti kuwa nzito na kuwa masculine na polycystic ovarian syndrome(PCOS) ukiangalia kwa maana hio wana mapungufu ya homoni za kike estrogen ijapokuwa kawaida anazo homoni zote ila zikiwa inbalance ndo inapelekea hali hio.Estrogen mi homoni muhimu kwenye mfumo mzima wa uzazi hata kutunga mimba na ukiwa na mapungufu nayo inaweza kupelekea kuyumbayumba kwenye mfumo wa uzazi!
 
Unataka kusema kwa sababu wa ndevu(homoni nyingi za kiume), mayai yao ni sperm? Sioni uhusiano.

Tanabahi: Sikupenda baoloji, kulikuwa na baridi kali sana.
 
Na wengine wasiozaa na hawana ndevu? Homoni zinakuwaje?

 
Na wengine wasiozaa na hawana ndevu? Homoni zinakuwaje?

Mimi nimeongelea wenye ndevu sio wasiozaa....kuna mambo mengi yanayoweza kupelekea mtu asizae ukiachilia mbali hormon inbalance
 

Nashukuru kwa mchango wako mkuu
 
Mwenye uelewa na hili tafadhali atujulishe itakua msaada kwangu na kwa wengne
Hakuna uhusiano wowote ule kati ya mwanamke kuwa na ndevu au kuzaa ama kutozaa

Ngoja niwaite Madr. waje watusaidie. Wapi Dr. @mimi49 , Dr. Mummy measkron, Dr. Riwa, Dr. hippocratessocrates, Dr. MziziMkavu, Dr.Mo na wengineo.
hujambo bibie charminglady

KWA IMANI YANGU MIMI MWANAMKE KUWA NA NDEVU NI ISHARA YA:

MAANA YA NDEVU KWA MWANAMKE:



Kuwa na ndevu kwa mwanamke ni dalili ya kupata fedha au mali au kupata heshima na kutukuzwa katika jamii au kupata cheo au kupata mafanikio au kupata Mamlaka.


Kama ndevu hizo zimeota upande mmoja, hiyo ni ishara ya kwamba utafanya kazi ya kuweka fedha ambazo mwisho wake zitapotea au utatapeliwa, unatakiwa uwe muangalifu sana.


Kama ndevu hizo zikiwa zimeota sehemu mbili yaani upande mmoja wa shavu na upande wa pili, hiyo ni ishara ya kufunguka kwa mambo yako yaliyokwama kwa muda mrefu.


Kama ndevu hizo zikiwa nyeusi, hiyo ni dalili ya mafanikio na kuridhika kimaisha na kuongezeka kipato chako.


Kama ndevu hizo zikiwa zimechanganyika rangi mfano zipo nyeusi, nyeupe na za rangi nyingine, hiyo ni ishara ya kufikwa na umasikini au balaa.


Kama rangi ya ndevu hizo ikiwa ni ya dhahabu au rangi ya Blonde, hiyo ni ishara ya kupata wasiwasi au kutishwa. Vile vile utapoteza heshima yako na inawezekana ukapoteza nusu ya utajiri wako.


Kama ndevu zikiwa chache zinazohesabika au zimepunguzwa, hiyo ni dalili ya kupata heshima kwa mumeo mpenzi wako au watu wako unaofanya nao kazi au biashara.


Kama ukiwa umeota ndevu nyingi kwa wakati mmoja, hiyo ni dalili ya kumpoteza mumeo aidha kukutoroka, kukuacha au kufa, na kama hayo yamekutokea basi utapata mume mpya au mchumba mpya.


Kama ukiwa mjamzito na ukaota ndevu, hiyo ni dalili kwamba utazaa mtoto wa kiume na kama ulikuwa na ugomvi au kesi basi itakwisha na utashinda.


Mwanamke kuota ndevu vile vile ni ishara ya kupata kazi, au kupata biashara, au kupata nguo mpya au kupoteza kitu au jambo kuharibika.


Kama umeota ndevu chache na zote zikiwa nyeupe, hiyo ni ishara ya kupata maradhi na kudhoofika kiafya.

Mimi Ninampenda Sana Mwanamke mwenye ndevu.
 

Attachments

  • mama ndevu.jpg
    5.8 KB · Views: 424
Mama ndevu!!!




Na Dunstan Shekidele, Morogoro.



Muhudumu mmoja wa baa maarufu ya Pema iliyopo eneo la Lunna mkoni hapa, aliyefahamika kwa jina moja la Asha, ambaye amejaliwa na mola kuwa na ndevu nyingi kama mwanaume, ameamua kutozinyoa ndevu hizo na kuziachia bila hiyana.

Mwandishi wetu, mwishoni mwa wiki hii, alimshuhudia mwana mama huyo akipiga kazi bila noma yoyote ambapo baadhi ya wateja wageni walionekana kumshangaa.

Alipotakiwa kuzungumzia uamuzi wake wa kitozinyoa ndevu hizo, Bi Asha alijibu kwa mkato kwamba yeye ni mke wa mtu na kwamba suala ya kuziacha ndevu hizo ni uamuzi wake na mumewe. Baa ya Pema ni miongoni mwa baa maarufu mkoni Mororgoro na zinozopendwa na mapedeshee wengi wa mkoa.



Kutoka Global Publishers Tanzania
 
Ngoja niwaite Madr. waje watusaidie. Wapi Dr. @mimi49 , Dr. Mummy measkron, Dr. Riwa, Dr. hippocratessocrates, Dr. MziziMkavu, Dr.Mo na wengineo.



I concur.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…