Ndio vina uhusiano hasa katika kuandika tarasimu...kwa mfano hii ni tarasimu ya kuvuta pesa mwilini mwako imeandikwa na wino wa peni hiyo na kufukizwa na udi huo..Ni shirki kama shirki zingine na shirki siku zote huwa ni dhambi do at your own risk
View attachment 2531600
Well hiki unachofanya sio sahihi na sio sawa kwa maana unahamasisha watu wenye uelewa mdogo kuhusu mambo haya kuthubutu kufanya kitu wasichokijua kwanza umeanza na mkwala kwamba hii ni shirki lakini ajabu mwisho wa siku unafundisha watu kuwa wakifanya watapata nini?
Kwenye hali ya sasa hivi ambayo mtu hawazi haramu wala halali unaweka sanaa yoyote ile lazima atathubutu tu. Wapo watakao kufuata PM na kukuomba uwape maelezo kamili kisha baada ya hapo utaigiza kama vile sio muhusika na baadae utataka uwadirect kwa muhusika na kutoa ladha nzima ya kile ulichopost na kunadi kwamba ni SHIRKI na unajikuta wewe ni agent wa hiyo shirki.
Nimekukosoa wewe kama umekasirika tukana sijali.
Kisha namkosoa aliyekuonyesha ama kukupa hii kitu na kudai kwamba inavuta pesa. Ikivuta pesa niite mbwa nimekaa hapa kwenye quote yako.
JIBU LA KIMAARIFA:
Kwanza kabisa hii sio talasimu ya kuvuta pesa haina ukweli wowote na ina madhara kwa asilimia 99.99%.
tuitizame,
Tukianza Ina shamsi katikati yaani alama ya kuwakilisha jua ambayo ni nishati ya kila kiiumbe hai na ambacho kisicho hai na inawakilishwa na nyota ya pembe tano ambayo ni utawala wa jumapili yenye thamani ya herufi F kwa maana ya Jina la Mwenyezi Mungu Farid (MMOJA) nyota yenyewe imekaa upande ikielekea zaidi upande wa kushoto imechorwa kwa wino wa blue ambayo ni rangi kinzani ya jua na pia na wino uliotumika ni wa kalamu za chemical ambazo hazina uhusiano wowote na buhuri zilizopo katika sayari (nyota) ya jua.
Pili: Jina linalozunguka hapo HASHAMSHAHAYNI ambalo ni jina la jini anayetawaliwa na watumishi wa malaika Izrael (Azrael) malaika mtoa roho za watu hivyo utawala wa mkuu wao wa chini ni Abu muhriz Al Hamar katika majini na Phaleg katika mashetani uandishi uliotumika hapo ni wa MIRIKHI ambayo ni utawala wa DAMU,MAAFA,VITA na MAANGAMIZI.
Tatu; Shikeli iliyotumika hapo ni
Amisio ambayo ni kinyume cha
Aquisto hivyo;
Amisio ni shikeli ya kukosa na Aquisto ni shikeli ya Kupata
Nne; Mpangilio wa talasimu za sayari hapo juu ni FA JA ZA kisha zikamalizikia na SHA KHA ZA moja kwa moja ni baina ya sayari 6 katika mpangilio wa vurugu jua mwezi na zuhura kwa pamoja na Jua Mushtara na Zuhura.
TARGET YA TALASIMU HII:
Hii talasimu malengo yake ni kumfilisi yeyote yule atakaye kuwa nayo na hatapata mafanikio na mafanikio kwake ayaone kama ukoma kila fursa awe anaiona ni tatizo,
Hii mlenga alitaka kumpa mlengwa ili afilisike ama aweze kufa maskini.
HITIMISHO 1:
yaani mtizamo wa talasimu hili ni vijakazi wamekuwa wafalme na wafalme wamekuwa vijakazi. Hana tofauti na mtu mwenye kusema baba alale na mtoto na mtoto alale na mama kingono hapo utakuwa umetukana familia ya watu. watakachokufanya mbona utaenda kuchekea chooni.
HITIMISHO 2:
Msipeane vitu msivyovijua maana zake kwa maana mtaleteana matatizo wenyewe kwa wenyewe Imagine mwenye kubeba talasimu hii hana tofauti na muandamanaji aliyebeba bango la kutukana uongozi wenye hasira kali na watu kama yeye.
Ukitumia talasimu malengo yake na results huanza hapo hapo unapokuwa umeipokea sasa embu kaa nayo muda fulani kisha utaona mbivu na mbichi mwenye kuishi miaka alfu moja hana tatizo kukusubiri ujisahau ukifika miaka arobaini na tano ili akuchekeshee chooni. watu wengi wanajiangamiza wao na familia zao kwa kushiriki wasio yajua.
Binafsi sishauri mtu apokee kitu pasipokuwa na msaada wa wenye kujua.
Rakims