Kuna ukweli kuhusu hili wakuu?

Kuna ukweli kuhusu hili wakuu?

machiaveli

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
2,225
Reaction score
5,055
Habari zenu wakuu?

Eti kwamba mwanaume ukiwa na msongo wa mawazo (stress) unapaswa kulia machozi kwamba inasaidia kukutuliza na kukuepusha magonjwa ya afya ya akili?

Iko hivi ndani ya miaka mitatu hii Kuanzia 2021 nilipata changamoto mbalimbali kubwa kwa vipindi vifupi vifupi
Mama wa watoto wangu alifariki,kikapata ajali,mzee wangu akaumwa,nikakosa kazi na changamoto zikazidi kujichanganya! Hata hivyo nilijitahidi KUPAMBANA nilikua ni sehemu ya maisha na yatapita tu kwani Kila mtu ana changamoto zake!!

Kuna wakati huwa nikitulia mahali napatwa na msongo ila napotezea nanyonga shada zangu navuta najisikia vizuri naendelea kuwatafutia watoto wangu ugali ukiwa Mimi ni baba na mama kwa mpigo

Kuna wanasaikolojia naskia wanasema mwanaume anapaswa kulia kutoa sumu, juzi kati nimejifungia ndani peke yangu nikijaribu kulia kwa kweli nilishindwa nikajikuta macho makavu nikajiona mpumbavu nikaanza kujicheka

NB:Mimi sikumbuki mara ya kulia ni lini,hata shule nilikua nikichapwa silii walimu wakasema huyu mtoto ni mkorofi
 
Hiyo kazi kwa yule chawa mbona easy tu! anauwezo wa kujaza djaba la machozi kwa siku tatu tu.
 
Dah pole japo yalishapita .
Wataalamu wanadai hivyo ila kwangu maumivu labda niamue kuyaachia mwenyewe toka moyoni na sio kwa kulia tu eti nilie yatoke..wapi!

Niamue niseme sasa basi staki umivu hili na itakuwa basi kwelikweli.
 
Sidhani kama kulia tu pekee, bali ni muhimu kufanya therapy inaisaidia kukuponyesha maumivu na kuondoa msongo. Hivyo tafuta mwanasaikolojia ambae ni mtaalam wa therapy.

Wao wanajua pakuanzia, pengine bado una maumivu au kuna mambo hujayakubali itakusaidia kuunguza dukuduku na maumivu moyoni taratibu ili kuweza kukubaliana na hali yako na kuendelea na maisha.
 
Dawa ya kwanza ni ku socialize kaka. Pamoja na maumivu yoooote maisha lazima yaendelee! Naomba nikusaidie kwa ufupi sana, AMKA PANGUSA NGUO SONGA MBELE. Najua ni ngumu ila amini unaweza!

Nimesoma yote uliyoandika nikatabasam tu ........

Nimepitia yote hayo mule mule tena kwa ugumu kuliko wako mkuu maana my wife wangu alifariki wakati anajifungua katoto kangu ka pili so aliniachia kichanga wa wiki! Na baada ya miezi 4 nikapoteza kazi .......na baada ya miezi 8 tu nikapiga mzinga wa maana haswa mikono mbende mbende wakati nauguza majanga ya ajali msenge mmoja kanifungulia bonge la kesi la uwongo nikasota sana, sasa fikiria huna kazi wewe ndio baba wewe ndio mama alafu bonge la kesi na mikono yote ime palalaizi una mabandeji na unawajua polisi wa bongo wasivyo bina-adamu

Hapo sijakwambia baada tu ya mazishi nikaingiliwa na majambazi wakabeba kila kitu hadi vyeti vya shule tangu vya chekechea hadi University mbwa wale

Ila amini nakwambia sasa hivi nimesimama balaa nguzo ya umeme inasubiri. Ni uchungu tu wa kumkumbuka kipenzi changu
 
Kutoa dukuduku ni moja ya tiba kubwa sana,,mfano umeona kumbe sio wewe peke yako unayepitia au uliyepitia machungu,,kuna mwamba hapo ametoa ushuhuda jinsi alivyopitia machungu zaidi yako,,hiyo inasaidia kujua kuwa kuna wenzako kama wewe pia

Pili hisia za machungu au msongo hauondolewi na pombe au bangi unachofanya ni kuahirisha tatizo lkn stimu zikiisha tatizo liko pale pale

Wanashauri wataalamu hisia za machungu zikikujia husizikwepe kwa maana kama utahisi kulia basi lia na kama kuhuzunika basi huzunika,kwa kufanya hivyo zinapunguza makali na kuchukuliwa na subconscious mind yako kwamba hizo hisia sio tishio tena kwako hivyo zinakuwa familiar kwako na baada ya mda fulani kupita utakuwa okay

Kuhusu kipenz chako uliyempoteza kubali kwamba ni kazi ya mungu na mda wake ulifika,usijiweke katika lawama labda kama hasingeshika mimba huenda angekuwa hai,,hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuondoka kwake

Kwahiyo maisha ndiyo yalivyo chief,,,lakini kama walivyosema wadau kama unahisi msongo unakuwa mkubwa waone wataalamu wakusaidie zaidi
 
Kufiwa na mke halafu watoto Bado wadogo au hata wakubwa hiyo mungu aepushe aiseh!

Pole sana Man!!

Usije dumbukia shimoni,mara nyingi msongo kama huo unaweza jikuta kwa mwanamke mbinafsi Sana akakuharibia maisha!
 
Yah man kwa Sasa sina wazo hata chembe la kutafuta mwanamke mwingine wa kuishi nae! Sitaki kujaza mambo mengine kichwani nashukuru watoto ni wakubwa wanaelewa ninayoyapitia hivyo na wao wamejivika uhalisia wanajua tunayopitia!
Mimi nachopenda niwaone madogo wanakua vizuri kama watoto wengine na Mimi pia niwe na nguvu na ufahamu wa kuwashika mikono
 
Kutoa dukuduku ni moja ya tiba kubwa sana,,mfano umeona kumbe sio wewe peke yako unayepitia au uliyepitia machungu,,kuna mwamba hapo ametoa ushuhuda jinsi alivyopitia machungu zaidi yako,,hiyo inasaidia kujua kuwa kuna wenzako kama wewe pia

Pili hisia za machungu au msongo hauondolewi na pombe au bangi unachofanya ni kuahirisha tatizo lkn stimu zikiisha tatizo liko pale pale

Wanashauri wataalamu hisia za machungu zikikujia husizikwepe kwa maana kama utahisi kulia basi lia na kama kuhuzunika basi huzunika,kwa kufanya hivyo zinapunguza makali na kuchukuliwa na subconscious mind yako kwamba hizo hisia sio tishio tena kwako hivyo zinakuwa familiar kwako na baada ya mda fulani kupita utakuwa okay

Kuhusu kipenz chako uliyempoteza kubali kwamba ni kazi ya mungu na mda wake ulifika,usijiweke katika lawama labda kama hasingeshika mimba huenda angekuwa hai,,hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuondoka kwake

Kwahiyo maisha ndiyo yalivyo chief,,,lakini kama walivyosema wadau kama unahisi msongo unakuwa mkubwa waone wataalamu wakusaidie zaidi
Pamoja sana mkuu
 
Back
Top Bottom