Kuna ukweli kukiwa na serikali ya majimbo ndio mwanzo wa kuigawa Tanzania kwa misingi ya ukabila na dini ?

Kuna ukweli kukiwa na serikali ya majimbo ndio mwanzo wa kuigawa Tanzania kwa misingi ya ukabila na dini ?

Wataalam wa politics, kuna ukweli kiasi gani kwamba kila jimbo likiwa na serikali yake kutachochea ukabila ?

Mfano kwa hapa Tz kila mkoa uwe na serikali yake
Shinyanga tumezalisha Almasi miaka yote hiyo tangu utawala wa Mwalimu lakini hakuna Stand ya mabasi ya maana, Bora hii nchi igawanywe kimajimbo Kila sehemu ineemeke kivyake.
 
Mfano kwa hapa Tanzania kila mkoa uwe na serikali yake, kuna ukweli gani itachochea ukabila au udini ?

..sio kila mkoa.

..ni kila JIMBO.

..Na hakuna jimbo ambako wanaishi kabila moja.

..kabla ya mikoa kuundwa, Tanganyika ilikuwa imegawanywa ktk majimbo nane kama sikosei.

..Na kipindi hicho hakukuwa na ukabila kwani tuliweza kupigania uhuru wa Tanganyika kwa umoja bila kubaguana kikabila.
 
Sio kweli, mikoa karibia yote ina makabila zaidi ya matano. Pia jimbo moja linaweza kuundwa na mikoa miwili, mitatu au zaidi.
 
..sio kila mkoa.

..ni kila JIMBO.

..Na hakuna jimbo ambako wanaishi kabila moja.

..kabla ya mikoa kuundwa, Tanganyika ilikuwa imegawanywa ktk majimbo nane kama sikosei.

..Na kipindi hicho hakukuwa na ukabila kwani tuliweza kupigania uhuru wa Tanganyika kwa umoja bila kubaguana kikabila.
Kwa Tanzania tukifuata huu mfumo itabidi majimbo yawe mikoa badala ya wilaya / halmashauri

Kenya kuna majimbo 47 yakiwemo Nairobi na Mombasa ambayo ni kama mikoa kwa Tanzania.
 
Huu mfumo unafaa sana asee.Kuna mikoa inatoa rasilimali nyingi lakini wana hali mbaya kuanzia uchumi,miundombinu mpaka elimu.
Kuna mikoa haiendelei kwasababu ya upigaji na wapigaji watu wake, Pesa zinatolewa kuendeleza miradi, zinaishia mifukoni mwa madiwani, halmashauri, chama ngazi ya mkoa, n.k.

Mfano mdogo ni Bukoba, wametoa mawaziri kibao wenye power ya kupanga bajeti lakini mkoa hauna maendeleo ila ni hao wabunge wanaita milioni 50 pesa ya mboga,hizo pesa za mboga wanatoa wapi ?
 
Kuna mikoa haiendelei kwasababu ya upigaji, Pesa zinatolewa kuendeleza miradi, zinaishia mifukoni mwa madiwani, halmashauri, chama ngazi ya mkoa, n.k.

Mfano mdogo ni Bukoba, wametoa mawaziri kibao wenye power ya kupanga bajeti lakini mkoa hauna maendeleo ila ni hao mawaziri wanaita milioni 50 pesa ya mboga
Upigaji ni tatizo mtambuka kwa nchi nzima.

Wahaya mkoa wao umepauka bwana asikwambie mtu,wana ardhi nzuri yenye rutuba,hali ya hewa mwanana kabisa lakini mkoa umefubaa sana.
 
Upigaji ni tatizo mtambuka kwa nchi nzima.

Wahaya mkoa wao umepauka bwana asikwambie mtu,wana ardhi nzuri yenye rutuba,hali ya hewa mwanana kabisa lakini mkoa umefubaa sana.
Upigaji ni tatizo ila viwango vimetofautiana, Kama mbunge kapata nyadhifa nzito ya uwaziri na bado kashindwa kusimamia miradi jimbo lake au kapiga pesa za miradi, hilo tatizo haliwezi kutatuliwa na serikali ya majimbo.

Halafu serikali ya majimbo ndiko kuna ufisadi zaidi,
 
Acha kuwaamini vilaza waliojazana si si emu. Hata kwenye uraia pacha ukiwauliza sababu za kuupinga, utaisha tu kucheka kwa dharau na kutikisa kichwa.
 
Back
Top Bottom