Kuna ukweli upi kati ya mambo haya mawili

felakuti

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
659
Reaction score
1,207
Je, katika mambo haya mawili ni lipi Lina ukweli?

Unakuta unataka kufanya jambo, katika kukaribia kulikamilisha, unapata hofu na woga sana, hatimaye unaacha.

Kwingine unataka kufanya jambo katika kukaribia kulikamilisha unakua hauna hofu Wala kua na wasiwasi

Sasa wataalam wa mambo ya kiroho wanasema ukiona jambo ambalo umechukua maamuzi ya kulifanya ambalo ni halali ukapata hofu na wasiwasi, basi hio njia ndio njia sahihi na itakayokufanikishia malengo yako, ila ukiona haupati wasiwasi Wala hofu ujue hio njia sio sahihi.

Je, wewe umeshapata Hali kama hii ?
 
Kwa Muktadha wa Kibiblia naweza kusema hivi!

Kuna muda ambapo mtu anataka kufanya jambo, lakini gafla anapoteza amani, Raha (rest) anaingiwa na hofu kubwa ... Hii Kibiblia ni ishara kuwa Hilo jambo si sahihi kulifanya.

Kumbuka jambo linaweza kuwa zuri lakini lisiwe sahihi!

Kuna muda mtu anapata amani ya Kufanya jambo, ila unapokaribia kulikamilisha gafla unapata hofu, unakosa Raha na wasiwasi ... Hii ni ishara kukujulisha kuwa unatakosea katika ukamilishaji wa jambo Hilo!

Biblia inasema ... Amani ya Kristo ndio ifanye maamuzi ndani ya mioyo wa watu!

Lakini pia inasisitiza kuitafuta amani na kuifuata!

Kila hofu, uwoga ni ishara! Na Kila ishara Ina ujumbe ndani yake!

Kikubwa si kuifuata hofu au wasiwasi Bali kuweza kuujua ujumbe unalotwa na hofu au wasiwasi!

Kwa mfano; Umeshawahi Kukutana na hofu na wasiwasi kubwa sana kabla ya Kufanya jambo! Mfano safari, kukubali ombi la mtu n.k! Lakini ukapuuuzia?

Na gafla huko mbeleni ukakutana na maumivu, ajali au hasara!

Ndio hii unasikia watu wanasema "Yaani mwili ulikuwa ulikuwa unakataa kwenda! Au moyo ulikuwa mzito sana"
 
Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi mzuri sana
 
Back
Top Bottom