Kwa Muktadha wa Kibiblia naweza kusema hivi!
Kuna muda ambapo mtu anataka kufanya jambo, lakini gafla anapoteza amani, Raha (rest) anaingiwa na hofu kubwa ... Hii Kibiblia ni ishara kuwa Hilo jambo si sahihi kulifanya.
Kumbuka jambo linaweza kuwa zuri lakini lisiwe sahihi!
Kuna muda mtu anapata amani ya Kufanya jambo, ila unapokaribia kulikamilisha gafla unapata hofu, unakosa Raha na wasiwasi ... Hii ni ishara kukujulisha kuwa unatakosea katika ukamilishaji wa jambo Hilo!
Biblia inasema ... Amani ya Kristo ndio ifanye maamuzi ndani ya mioyo wa watu!
Lakini pia inasisitiza kuitafuta amani na kuifuata!
Kila hofu, uwoga ni ishara! Na Kila ishara Ina ujumbe ndani yake!
Kikubwa si kuifuata hofu au wasiwasi Bali kuweza kuujua ujumbe unalotwa na hofu au wasiwasi!
Kwa mfano; Umeshawahi Kukutana na hofu na wasiwasi kubwa sana kabla ya Kufanya jambo! Mfano safari, kukubali ombi la mtu n.k! Lakini ukapuuuzia?
Na gafla huko mbeleni ukakutana na maumivu, ajali au hasara!
Ndio hii unasikia watu wanasema "Yaani mwili ulikuwa ulikuwa unakataa kwenda! Au moyo ulikuwa mzito sana"