Kuna ukweli wowote juu ya zuio la usajili wa Noah zinazobeba abiria Moshi - Tarakea?

Justine_Dannie

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
1,962
Reaction score
1,618
Habari,

Hivi karibuni nimekua najipanga kuingia kibiashara ya usafirishaji kwa maana kununua Noah na kuitumia kutengeneza kipato cha ziada pamoja na kumtoa dogo mtaani bila ya lakufanya (jobless).

Sasa kuna waungwana hapa ndani alinipa taarifa kwamba gari aina ya Toyota Noah zimezuiliwa kusajiliwa.

Yaani zilizopo zinatosha na hawasajili zozote mpya kwa sasa isipokua kuna aina nyingine ya magari ndio wanayapokea na kigezo kikubwa kikiwa ni suala la usalama.

Naomba mnisaidie kwa upana wa taarifa hizi na ukweli wake;
1: Ni kweli zimesitishiwa usajili?
2:Kama 1 ni kweli) je ni aina gani hiyo mpya ya gari zinazohitajika kwa sasa?

Asanteni:

J.D.D.M
 
Piga simu office ya usalama barabarani mkoa RTO tafuta namba kwenye mtandao,
Nimeongea nae leo akaniambia hilo Ni jukumu la SUMATRA,
Lakini pia hata kungelikuwepo na taarifa za kuzuia hizi Noah mpya kuingia katika biashara, taarifa wangepata wao pia maana wanahusika Moja kwa Moja na utekelezwaji wa Sheria.
Mwisho ajamaliza na kuita ni uzushi.
Je step two nionge na watu wa Sumatra Kilimanjaro?
 
Cheki na sumatra mkoa ili kujiridhisha.
 
Kaka nimeongea na wahusika na hatimae kupata majibu,
Hivyo Ni kweli kwamba kwa sasa hawatoi license kwa Noah ya route hiyo. Isipokua zinazohudumu zitaendelea mpaka zitakapoondoka kwenye mzunguko huo,
Lkn wanatoa license kwa Noah zinazofanya route kwenye feeder road .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…