Kusema ukweli kama Utalii ukipewa nguvu na watu wakajua umuhimu wake unaweza kuchangia bajeti kubwa kuliko sekta nyingine yoyote kutokana na vyanzo vya kitalii tulivyonavyo ukilinganisha na nchi nyingine Duniani.Tabu ipi?hakuna ambaye hatambui uhusiano wa biashara ya ndege na utalii ni kama mume na mke.Leo hii kwa mwaka moja watalii wanaoingia Tanzania ni chini ya milioni moja ukilinganisha na nchi zingine ambazo vyanzo vya kitalii ni vichache.Kutokana na vyanzo vyetu kwa mwaka inapaswa kuingia watalii wasiopungua milioni 5.Wazee walinena huwezi kujua future wakati haujui past ilikuwaje
Hatupendi kujifunza kutokana na makosa
Biashara ya ndege ni biashara yenye risk kubwa sana na hasa ukizingatia ndege ndiyo injini kuu kwenye hii biashara lakini kwa kipindi kirefu kumekuwa na matatizo mengi katika uendeshaji wa hili shirika.
MATATIZO:
1)Huwezi kuendesha shirika la ndege na kuleta faida nzuri kama ni part ya siasa.Siasa siku zote lazima iwe peke yake na biashara iwe peke yake japo vyote vinaweza kuwa ndugu lazima sumu kubwa kwenye biashara ni kumuachia ndugu aiongoze biashara siku za usoni hautajua mchawi wako ni nani
2)Uendeshaji wa shirika la ndege ni mithili ya timu ya mpira.Timu ya mpira si jina bali ni wachezaji huwezi kusema unaanzisha timu wakati hujui nani atacheza.Hiyo haiwezi kuwa timu na hata upatikanaji wa wachezaji lazima uwaandae.Huwezi ukaendesha shirika la ndege ambalo litaleta faida mathubuti kama hujawekeza kwenye watu.Leo hii tunasomesha mainjinia wa ndege South Africa ambao kila mmoja gharama yake ni dola laki moja je tutasemesha wangapi ili tupte watu wa kutosha.Tangu mwanzo kama shirika llilipaswa kuisukuma serikali kujenga chuo kikuu cha masuala ya Aviation and Aerospace engineer ambacho kingeandaa wataalam mathubuthi katika fani mbalimbali ikiwemo Airline management and organization of airline enterproses watalaam hawa wamekosekana na ndiyo maana matokeo yake tumeyaona
3)Shirika kama shirika lazima liundwe na timu ya watalaam waliobobea katika masuala ya uendeshaji wa mashirika ya ndege watu kama CEO wana play role kubwa sana tatizo kubwa kumekuwa hakuna njia mbadala wa kuwapata hawa watu.Ukiangalia kwenye matangazo ya kazi za serikali utakuta CEO lazima uwe umefanya kazi miaka 10 kitu kimoja hatutatumbia kuwa na uzoefu mkbwa katika eneo Fulani haimaanishi wewe ni innovative.Mashirika ya ndege ni sensitive sana hapa hatuongelei mashirika ya kilimo.Tunaongelea mashirika yenye assets ambazo risk yake kubwa sana mfano ajali
SULUHISHO
Nchi kama nchi inahitaji sana kuwa na shirika la ndege kwani ni chanzo kizuri cha mapato na ajira.Mashirika kama haya ni rahisi kutoa ajira zaidi ya 10000 mfano mdogo Ethiopian airline imetoa ajira za kudumu 17000 na bado inaongeza idadi kwa siku za usoni
Hakuna kinachoshindikana chini ya jua
1) Lazima upatikane uongozi wenye kujua nini unafanya na nini unataka kuachive.Mfano kwa CEO asipatikane eti kwa kuwa amefanya Air Tanzania kwa miaka ishirini hayo ni makosa.CEO apatikane kwa international biding itangazwe nafasi pote duniani ili kupata mtu mwenye greatest archivement kwenye uendeshaji wa ndege potelea mbali watume CV watu 10000 lakini achaguliwe mmoja tu.Na huyu mtu afanye kazi kwa mkataba wa miaka miwili akishindwa kufikia malengo basi anaachi kiti.Mimi sioni tabu kama leo tukimlipa hata dola za kimarekani laki mbili CEo anayeweza kuingiza faida ya dola milioni 500 kwa mwaka.Mfano mdogo tuangalie club kubwa za mpira wa miguu duniani kocha haijali kuingia mkataba na kocha wa milioni 20 dolla ili elete ushindi akishindwa straight away anaachia kiti kuwapa watu wenye uwezo
Tukishindwa kumpata CEO kwa njia hii basi tuangalie airline gani imefanya vizuri zaidi duniani tumface CEO wao tumpe dau zaidi ili aje kufanya wonders and this is what we call business hakuna undugu na sio jambo geni wakati Bill Gate alipoanzisha Cascade investment wapi alipata fund manager ambaye alimuingizia faida kubwa zaidi?alimchukua kutoka kwenye kampuni nyingine na kumuongeza dau kwa upande mwingine ndivyo thamani ya ahira inavyotakiwa kuwa
2.Shirika letu linapaswakuwa na vision plan kwa mfano malengo ya miaka 10,malengo yamiaka 20.Hili litachochea kazi ya watu kuhakikishia wanafikia malengo mfano malengo ya miaka mitano kutua kwenye viwanja vyote Africa na siyo tu kutua bali kuwa na kiwango cha faida ambacho shirika litapigana kufa na kupona ili lifikie kiwango
3.Ili kulifufua shirika tunaweza kuanza na ndege zenye daraja moja tu pili lazime watumie ndege zenye umbo jembaba kwa kizungu (short-haul flights which complements the range of
narrow-body)Kwa nini hizi ni bora kwa mashirika yetu gharama za uendeshaji wake ziko chini ukilinganisha na ndege zenye maumbo mapana kwa mfano kwa kuanzia shirika letu linaweza hata kuanza na ndege kumi aina ya Sukhoi Superjet 100 capacity yake ni abiria 100 kwa sasa bei ya ndege moja ni dola za kimarekani milioni 35 sifa za hizi ndege ni unafuu wa gharama katika uendeshaji
4 Shirika lazima liachane na tabia ya kukodi ndege kukodi ndege moja ya airbus kama linavyofanya kwa sasa gharama zake ni milioni nne dola za kimarekani hakuna umuhimu lijikusanye hata kwa mikopo lipate ndege zake
5)Faida za kununua ndege kwa uwingi(bulk procurement) kuna discount kubwa inatolewa na isitoshe ndege mpya pia ni nafuu zaidi kuziendesha hazina matatizo ya kiufundi pia kuna efficient interm of fuel,training,maintanance pili shirika kama lilinunua ndege hizi kwa discount linaweza kuzitumia kwa muda wa miaka 10 then likaziuza kwa bei kubwa hapo tunazidi kuongelea faida
6)Pia kuna gharama kubwa za kuendesha airline kupitia traditional hubs kama JK international airport kuna gharama nyingi kama handling nk shirika linaweza kuopt secondary hub (airport ndogo) mfano ndege inakwenda Rwanda sio lazima tutumie Kigali international airport inaweza kutumia airport ndogo karibu na Kigali kwa kawaida hizi zinaitwa secondary hub gharama zake za aircraft handling zipo chini sana ukilinganisha na viwanja vikubwa na pia ziingie mfumo unaitwa offload turnaround(yani ndege inafika inashusha na kugeuza)itaounguza gharama nyingi sana za kupack pale mpaka asubuhi
7)Mashirika mengi sana ya ndege yalikufa kutokana na gharama kubwa za mafuta ya ndege.Shirika lazima liwe na mikakati ya muda mrefu sana wa kibiashara.Moja lazima liwe na storage yake yenyewe yenye capacity kubwa sana mfano kipindi hiki wakati mafuta yameshuka sana duniani lazima inunue mafuta kwa wiki inadvance hata kwa miaka miwili kwa kufanya hivyo itaokoa pesa nyingi sana kwenye mafuta kwa kipndi chote hicho
7)Gharama zingine zinaweza kupunguza kwa kuanzisha database nzuri ambayo itaondoa ulazima wa kuwa na agent kila kitu kifanywe online bila ya kuwa na agenti au ofisi za ziada na gharama za majengo,kuwa na system ya wafanyakazi wenye kazi mbalimbali mfano hawa cabin crew wanaweza pia kucheki tiketi pale getini pamoja na kusafisha ndani ya ili kupunguza watu
Hayo ni machache tu ila yapo mambo mengi sana yanayoweza kulisimamisha shirika letu kidedea